Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Twiga, Hussein Mbululo (kulia) akitoa maelezo ya huduma mbalimbali zitolewazo na Benki hiyo wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kushirikisha taasisi zake zote. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Manazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Twiga, Hussein Mbululo akiwaonesha waandishi wa Habari Nishani ya Ulezi Bora wa Vikoba iliyotunukiwa Benki ya Twiga kwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo nchini. Mbululo alikuwa akiionesha wakati Benki hiyo wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kushirikisha taasisi zake zote. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Manazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Ofisa Masoko wa Twiga Bank, Adelbert Archard akiwagawia wanafunzi vipeperushi na kuwapa maelezo juu ya Akaunti maalum ya Akiba kwa watoto , walipotembelea banda la Benki hiyo wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kushirikisha taasisi zake zote. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Manazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...