Mdau Saleh Jaber (katikati) akiwa kazini kwake London akipeperusha bendera ya Tanzania katika siku maalum katika mwezi huu wa Black History Month. Saleh na wenzake wamechagua mwezi huu kukuza mfuko wa msaada kwa kusaidia Somalia Crisis Appeal na Anti-Slavery Charity uliyotayarishwa kazini kwao na kusimamiwa na mfanyakazi mwenzake Lyndon Haynes (kulia) ambaye ni mtunzi wa kitabu chaThis Functional Family ambacho kinapatikana Amazon, kulia kwa Saleh ni mfanyakazi mwenzake dada Bassey Henshaw.

Mwito wa mfuko huo ni "encouraging and promoting tolerance amongst ourselves, where differences should be understood and respected". Pesa zote ambazo zinakusanywa zitapelekwa kwenye mifuko miwili ifuatayo:http://www.savethechildren.org.uk/en/somalia-crisis.htmhttp://www.antislavery.org/english/what_we_do/default.aspxBonyeza kwenye link juu kuchangia upande wako.Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...