![]() |
Na Woinde Shizza
wa Globu ya Jamii, Arusha
JESHI la polisi mkoni Arusha, linamsaka msanii nguli wa kizazi kipya wa jijini Dar es salaam,Nasibu Abdul Juma almaarufu kama Diamond (pichani) kwa tuhuma za utapeli wa kujipatia kiasi cha shilingi milioni 1.5 na kushindwa kuhudhuria shoo jijini Arusha na kusababisha vurugu na uharibifu mkubwa wa mali katika ukumbi maarufu wa Triple A.
Diamond anadaiwa kuingia mkataba na kampuni ya Arbab Mb Entertaiment ya jijini Tanga kuja kufanya shoo Ijumaa oktoba 8 mwaka huu baada ya kukubaliana kulipwa ujira wa shilingi milioni 2.5.
Msanii huyo anatuhumiwa kuingia mitini na kushindwa kuhudhuria shoo hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutokana na kuachwa na ndege.
Kukosekana kwake kulisababisha vurugu kubwa katika ukumbi huo kutoka kwa mashabiki waliokuwa wakitaka kurudishiwa pesa zao za kiingilio,ambapo katika vurugu hizo wacheza shoo wa msanii huyo na mwandaaji wa shoo hio walitiwa mbaroni na polisi .
Taarifa zaidi zimeeleza kwamba msanii huyo alilipwa kiasi cha shilingi milioni 1.5 sanjari na kukatiwa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi yenye thamani ya shilingi laki 3 unusu,ambapo aliwatanguliza wacheza shoo wake wanane jijini Arusha.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kampuni ya Arba,Mbwana Imamu, alisema kuwa Diamond alishindwa kutokea na hakuwa ametoa taarifa yoyote ya kutofika kwake kwenye shoo hiyo na kwamba muda wote walipokuwa wakiwasiliana alikuwa akimwambia kuwa anakuja.
Ilipofika usiku wa manane bila msanii huyo kutokea, mashabiki waliokuwa wametoa kiingilio wapatao 2000 ndani ya ukumbi huo walianza kuleta fujo wakishinikiza kurudishiwa fedha za kiingilio kiasi cha shilingi 10,000 kila mmoja walizokuwa wamelipa.
Vurugu hizo ziliambatana na uvunjwaji wa viti, chupa, Glass, vioo na samani mbalimbali za ndani na watu kupigwa wakiwemo ma-DJ waliokuwa wakichezesha muziki.
Hata hivyo polisi waliarifiwa na kufika katika eneo hilo ambapo walimtia mbaroni mwandaaji wa shoo hiyo pamoja na wacheza shoo wanne kati ya wanane wa Diamond ambao bado wanashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi mjini hapa, huku polisi ikimtaka msanii huyo kujisalimisha kituoni hapo.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa The blue Triple A, Papa King alisema kuwa hasara iliyopatikana kutokana na vurugu hizo ni shilingi milioni 3.5 na kwamba imetia doa ukumbi huo unaoheshimika hapa nchini na Afrika mashariki.
Nae mkurugenzi wa Arbab Mbwana Imamu alisema kuwa msanii huyo amemtia hasara ya shilingi milioni 20 ambazo anamtaka kuzirudisha yakiwemo malipo ya uharibu wa ukumbi huo.
Diamond alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kuwa hakufanya maksudi kutohudhuria shoo hiyo, bali aliachwa na ndege iliyopangwa iondoke majira ya saa 12 jioni katika uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere jana.
Hata hivyo alisema kuwa yupo tayari kufanya shoo yoyote bure katika ukumbi huo ili kufidia hasara hiyo iliyotokea.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Afande Akili Mpwapwa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa bado wanawashikilia wacheza shoo wanne wa Diamond kutokana na kosa la kusababisha vurugu na auharibifu uliotokea katika ukumbi huo wa Triple A na Diamond anatakiwa kujisalimisha katika kituo hicho cha polisi jijini Arusha.
Mnauliza vurugu Arusha? Vijana wamechochewa, vurugu ni namna ya maisha na subira imeondoka. mPoleni msiokuwa na hatia!
ReplyDeletevurugu na kuvunjiwa sio shughuli ya mwimbaji.
ReplyDeletewenye venue ndio walipe kwa nini hawana security nzuri ambayo ingezuia mambo hayo?
hakuna haja ya kuwashikilia hao wengine next time fanyenyi booking ya early flights ili mtu aweze panda ndege inayofuata
pia waachieni wapambe wake amesema ataimba show tena bure waliokuwa na ticket wapewe chance ya kuingia tena lazima wanakitu cha kuthibitisha walinunua ticket
ok mwacheni nyie polisi hamna kazi za kwenda kukamata wezi mnakamata watu waimbaji
shame to u all
Kijana thamini kazi!!!
ReplyDeleteNo call no show! Kwanini hakusema mapema kuwa ndege imemuacha? Kijana hayuko serious na kazi.
ReplyDeleteau alikuwa na mtoto Wema hadi ndege ikamuacha?
ReplyDeleteanachezea nafasi huyo ngoja tu kidogo
ReplyDeleteasahaulike,,,,atajutia hizi nafasi,,ndo ulimbukeni wa mbagala,,,anajiona toff toffi
Haya we, hapo tu katangaza uchumba ameanza kulega lega je akioa, naamini userious wa maisha unapaswa kuanza kabla ya kuona ndo watu watajua uyaimbayo. But thou hata kama aliachwa na ndege angedrive angefika dar hata iwe late but aonekane
ReplyDeleteatakua kacheleweshwa na wema huyo. thamini kazi kijana
ReplyDeleteCommitment ndio rafiki wa mafanikio kijana, ama utaishi kama wale enzi zile.
ReplyDeleteWafanya vurugu wasilaumiwe ila wakulaumiwa ni muandaaji na msanii
KIJANA KOMAA NA RATIBA MAANA NDO MISINGI YA KUFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA GAME
ReplyDeleteHuo ni ulimbukeni tu, kwa nini achelewe ndege wakati alijua mapema kwamba alitakiwa kwenda kufanya shoo Arusha?
ReplyDeleteFedha alizichukuwa mapema kwa hivyo hakukuwa na sababu ya msingi.