Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abdulrahman Kasembe a.k.a Dulayo D-Timing (pichani) anatarajia kuwaongoza wasanii wengine kutoa burudani  katika usiku wa wanavyuo ujulikanao kama Bagamoyo Intercolleges Night.Pamoja na Dulayo kutakuwa na wasanii wengine wa muziki wa asili na muziki wa disko utakaoporomoshwa na dj Nature Skills.

Kwa mujibu wa bw. Kim Kimenya ,mkurugenzi wa kampuni ya Kimkev entertainment Dulayo anayetamba na nyimbo ya “Twende mchumba” ataburudisha kwenye usiku huo unaotarajiwa kufanyika kesho Ijumaa tarehe 28.10.2011 kuanzia saa 2:00 usiku katika ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na utamaduni Bagamoyo (Tasuba),ambapo tiketi za tukio hilo zinapatikana kwenye duka maarufu la nguo za kiume liitwalo Mrimi classic wear liliopo mjini Bagamoyo.

Kimenya alisema kuwa usiku huo ambao unafanyika kwa mara ya kwanza mjini Bagamoyo unatarajia kuhudhuriwa na wanavyuo wasiyopungua 1500 kutoka vyuo vya Bagamoyo na utakuwa usiku wa rangi nyeupe, ambapo watakaopendeza  kwa mavazi ya rangi nyeupe watazawadiwa fedha taslimu pamoja na kulala kwa usiku mmoja kwenye hoteli maarufu za mjini Bagamoyo.Sambamba na zawadi za waliopendeza pia kutakuwa na zawadi kwa atakayejibu swali la usiku huo ambaye  atajipatia fedha taslimu.

Kimenya amewahakikishia wapenda taaluma na burudani kuwa usiku huu umeandaliwa kwa umakini mkubwa,hivyo wategemee tulizo la mioyo yao kwa kuwa kwenye mikono salama ya waandaji na kupata burudani ya kihistoria katika mji wa Bagamoyo.

Usiku wa Bagamoyo intercolleges night ni usiku wa taaluma na burudani wenye lengo la kuwaunganisha na kuwaburudisha wanavyuo wa mji wa Bagamoyo na nje ya Bagamoyo.Pamoja na burudani wanavyuo watapata nafasi ya kuelezea na kujadili juu ya umuhimu wa kozi wanazojifunza kwa jamii.

www.kimkeventertaiment.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kazi kweli kweli wana Bagamoyo. Natumaini wadau watatimbwilika mpaka basi. Kama vile namwona PAPA KAWOGO, PAPA KIM, PAPA MARTIN DR, PAPA GISASI,NA MAPAPA WENGINE, Mungu awapeni nini jamani hiyo siku. Six atakosa kweli!!!!! we thumutuuuu. Big up Kim

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...