Mheshimiwa Waziri, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akipokea maelezo kutoka kwa Afisa ruzuku, Neil Ngala kuhusu mchango wa Shirika la The Foundation for Civil Society katika maendeleo ya jamii wakati alipotembelea banda la Shirika hilo kwenye maonyesho ya wizara hiyo katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi mmoja. Kushoto kwake ni Naibu Waziri na nyuma mwenye suti ni Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation, Bwana John Ulanga.The Foundation imealikwa kama mdau katika maendeleo ya jamii.
Mheshimiwa Waziri akiuliza swali kuhusu ruzuku zinazotolewa na namna ufuatiliaji unavyofanyika kuhakikisha zinatumika kama inavyotakiwa.
Baadhi ya wananchi waliotembela banda la The Foundation wakipata maelezo ya kazi zinazofanywa na Shirika hilo na mchango wake katika maendeleo ya jamii.
Wananchi wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Afisa Mawasiliano wa The Foundation, Mwanaidi Msangi wakati walipotembelea maonyesho hayo yanayoendeleo viwanja vya mnazi mmoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...