Maji yanaendelea kuwa bidhaa nadra sana nchini.Hali ya Mto Ruaha Mkubwa (The Great Ruaha) ambao unategemewa sana na mabwawa yanayotumiwa na Shirika la Ugavi wa umeme nchini Tanzania (Tanesco) ya Mtera,Kidatu na Kihansi kuzalisha nishati hiyo, uko katika hali mbaya sana na kwa hakika hakuna matumaini kabisa endapo kama mvua tarajiwa za masika zitachelewa kunyesha.
Historia ya hifadhi ya Ruaha haiwezi kutenganishwa na Mto Ruaha Mkuu au Mto Ruaha Mkubwa hivyo bila uwepo wa mto Ruaha Mkubwa, mimea na uoto mwingine wa asili utatoweka vivyo hivyo kwa wanyama ambao ni rasilimali kubwa ya Taifa la Tanzania.Kwa sasa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ni kubwa kuliko hifadhi yoyote nchini ikiwa na meta za mraba 20,000 (Elfu ishirini).
Ruaha pia ni ya pili kwa ukubwa barani Afrika ikifuata kwa karibu kwa hifadhi ya Salonga iliyoko nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya watu wa Congo.


hiyo kali ruaha ni hifadhi kubwa kuliko zote ikiwa na meta za mraba 20,000, huo ni uongo, au niseme kuna makosa kidogo hapo. ni ya pili kwa ukubwa, na very soon itakuwa ya tatu, kwa sasa ya kwanza ni serengeti 14000+km2 na ruaha ni 10000+km2
ReplyDeleteMkuu hapo unaweza ukawa sawa au siyo sawa inategemeana na wapi kila mmoja data alikozitoa: Mimi nadhani hapa suala siyo ukubwa au udogo wa hifadhi. Hapa ni issue ya utunzaji wa mazingira. Yaani mshikaji unaonyesha ni kwajinsi gani hauguswi na suala la uharibifu wa mazingira.Jamani watanzania tuamke tusipo kuwa na umakini, yatatukuta ya ukame wa somalia. Bila kuhifadhi uoto wa asili mvua itatoka wapi? Miti inakatwa kwenye misitu sisi tupo tunaangalia tuu. Tuige mfano wa wananchi wa Venezuela(kama sijakosea) ambao wameandamana kupinga ujenzi wa baraba inayotaka kupita katikati ya msitu mkubwa ambao kwao ndiyo chanzo cha mvua,na jamaa wanataka hata Rais wao ajiuzuru. Tukitunza misitu yetu Mvua zitanyesha, mabwawa yatajaa maji, umeme utapatikana kwa wingi na kwa gharama nafuu. Kama umeme ukipatikana kwa gharama nafuu watu watatumia umeme kupikia na kuachana na matumizi ya mkaa hivyo misitu itapona. Jamani nadhani Rais ajae aje na kauli mbiu ya MAZINGIRA KWANZA:
ReplyDeleteNi sawa ndugu yangu nilitaka kuweka data sawa, kuhusu mazingira nakuunga mkona kabisa lakini naona kama unawapigia mbuzi gitaa, wanasikiaga hao sasa? Swala la mzingira lianza na mtu mmoja mmoja, wengi wetu hatuyajali mazingira kabisa ndo maana hata miji yetu ni michafu sana. Tukifanikiwa kuweka mazingira safi na kuyatunza ndo tulichukulie swala la kitaifa. Ni kweli kabisa nchi inageuka jangwa, wengi wetu hatujali kutunza kitu ambacha hatumiliki sisi. Tumeweka siasa mpaka kwenye mazingira. Huyo rais wako anataka kujenga barabara ya lami serengeti, vigogo wengine ndio wameshamiri na biashara ya kuuza miti nje ya nchi, watanzania tunawashangilia. Vinaweza kuwa ni vitu vidogo sana lakini madhara yake tutayajutia kwa vizazi vingi vijavyo
ReplyDelete