Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Hussein Mponda akitoa hotuba ya kuzindua rasmi wiki ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika kusheherekea miaka 50 ya Uhuru ambapo pamoja na mambo mengine ameelezea vipaumbele vitakavyozingatiwa baada ya miaka 50 ya Uhuru kuwa ni pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma za Afya na Ustawi wa Jamii, Kuimarisha huduma za Afya ya Wanawake wajawazito, watoto wachanga na watoto wenye umri chini ya miaka 5 ikiwa ni pamoja na kuimarisha udhibiti wa magonjwa yanayoammbikiza na yasiyoambukiza pamoja na yale yaliyosahaulika.Pia ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kupima Bure Afya zao na kipindi chote cha wiki ya maadhimisho hayo itakayomalizika kesho Jumapili tarehe 2, Oktoba, 2011.
Home
Unlabelled
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YAZINDUA WIKI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...