Kuna watu wameshikilia 'REMOTE CONTROL'. Watu hawa wana uwezo wa kubadilisha channel wakati wowote wanapojisikia. wameupata wapi UWEZO huu? ni kutokana na MAARIFA na 'FREE WILL' aliyopewa binaadam. MAARIFA YANAYOMPA UWEZO WA KUTAMBUA NA KUJITAMBUA na FREE WILL inayompa uwezo wa kufanya lolote kulingana na utashi wa hayo MAARIFA yake.

Hili tatizo la hali mbaya ya maisha ya wakaazi wengi wa Dunia hakuna Rais wala Chama chenye uwezo wa kulitatua kutokana na ukweli huo wa kuwepo kwa watu walioshika hizo REMOTE CONTROL.

Hali hii itaendelea kwa muda mrefu mpaka tutafikia hatua ya kuwadharau viongozi na kuzidharau Serikali kama wafanyavyo watoto wanaomdharau baba mlevi anayejikojolea, anayevua nguo na kufanya VITUKO hadharani, baba asiyeiongoza familia yake zaidi ya kuiletea fedheha. ndivyo itakavyokuwa kwa wananchi dhidi ya serikali zao kutokana na ukweli kwamba hakuna mabadiliko chanya yanayoletwa na Serikali zao.

Baada ya muda, walioshika remote control wata-achia mirija na neema zitaanza kumwagika miongoni mwa jamii katika nchi nyingi, taratibu watu wataanza kuona mabadiliko katika huduma za jamii, wenye kupenda kufikiria watajiuliza mabadiliko haya yametokea wapi? mbona tumefuata misingi ya kidemokrasia na utawala bora na utawala wa sheria kwa miaka mingi lakini hakukuwa na mabadiliko? mbona rasilimali tumekuwa nazo kwa miaka mingi lakini hatukuwa na hali nzuri?

Wakati fikra hizo zikiwa zinaendelea miongoni mwa 'WAJINGA' wachache, taratibu kwa mbali kitaanza kusikika kinanda na ngoma kutokea mbali, midundo ambayo itaanza kusikiwa na WAVIVU wa kufikiri ambao kwa mbali wataanza kuchezesha miguu, mikono na hatimaye kichwa kabla ya kunyanyuka na kuanza kucheza kufuata midundo hii isiyojulikana inakotokea.

Taratibu tutaanza kufanywa tuamini kuwa mustakabali wa maisha yetu hautakiwi kumtegemea Mungu kabisa kwa sababu WATATUFANYA tuamini kuwa Mungu hakutusaidia wakati wa shida, WATATUFANYA TUANZE KUAMINI HAKUNA UUNGU, kama ambavyo wameshaanza kutufanya tuamini. kutokana na akili zetu nyingi na uwezo wetu mkubwa wa kufikiri tutajiuliza maswali ya msingi ambayo yatatupa majibu ya harakaharaka kuhusu shaka zetu dhidi ya utukufu wa MUUMBA.

Taratibu tutaanza kutoka misikitini na makanisani na kuanza kufuata njia zao...

Inaweza isitokee katika karne hizi, lakini ndiko tunakokwenda.

Nnamuomba aliyeniumba na kunipa yote haya ya ndani yangu na yanayonizunguka, yanayoonekana na yasiyoonekana kwa macho ya kawaida, anikinge na mkumbo huo utakaoangamiza wengi, Amin.

Mdau
Masoud.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. nimekuelewa vizuri Masoud na unayoyasema yote sahihi

    ReplyDelete
  2. Asante Masoud, ebana uko deep balaa.. wasioelewa poleni lakini mkirudia mnaweza pata maana ya hadithi hii!!

    ReplyDelete
  3. yes kaka this is a real critical thinking

    ReplyDelete
  4. Mdau Masoud hueleweki mbona.Unaonekana ni fearmonger.Nikweli kuna watu wanaleta fikra za upotoshi na kumnaka Mola Muumba lakini hueleweki unachotaka kusema.Weka wazi unachotaka kupresent ili wadau wakuelewe wachangie issue kwakukusapoti au kukupinga.Ila usiwatishe watu kwakauli zako zisizo wazi,huwezi sema watu wengi wtaangamia bila ku-elaborate.

    ReplyDelete
  5. Kwa nini watanzania tunashindwa kuandika kuhusu mada kwa kutaja moja kwa moja kitu tunachotaka kuzungumzia? Huwa tunaogopa kitu gani? Kwa nini huyu mwandishi anashindwa kusema wazi anachotaka kusema mpaka atumie mifano ya kitoto kama 'remote control' n.k?

    Kama ni Rais ndiye unaona hafanyi kama inavyotakiwa, basi sema Raisi Kikwete amekosea hapa na hapa, kama ni waziri basi sema waziri fulani kakosea pale, ili watu tunaosoma tuweze kukuelewa na kufaidika na maelezo yako. Hii uliyoandika hapa ni kama hadithi ambayo haimsaidii yeyote.

    ReplyDelete
  6. kitu anaongelea sii mtu mmoja au nchi moja bali ni watu fulani katika dunia hiii wanauwezo sanaaana, wamejiitayarisha vya kutosha kabda hata viinchi vyetu havijapata uhuru. Nahawa hawa watu ndo wanatuchezea na remoti cotrol watakavyo. mimi nazani ni kina world bank,IMF na havo mashirika mengine ya kimataifa yanayotupa mahela kwa mikopo na yametuzingira toka tupate uhuru mpaka leo na kesho. wao wanatoa masharti siye ndo twapokea lawama mwishowe

    ReplyDelete
  7. tatizo mtoa maoni wa nne na wa tano, mliishia kusoma magazeti na sasa mmehamia kwa issa michuzi na ndio mwisho wa upeo wenu. jitahidini msome vitabu, makala na majarida mbalimbali mjue kuwa kuna aina nyingi za uandishi. Napata picha kwanini tunasaini mikataba mibovu maana tukipindishwa kidogo tu imekula kwetu. Mmeaibisha jamii na familia zenu

    ReplyDelete
  8. Kaka napenda kukushukuru sana kwa maada uliyoitoa leo, mimi binafsi ni muumini wa dini ya kikristo na yote uliyoyazungumzia yamezungumziwa kwenye biblia kwa yatakayotokana nyakati za mwisho. watu watamkana Muumba(Mungu) na kuabudu watu na miungu na huo ndio utakuwa utawala wa shetani kabla ya hukumu ile ya Mwisho. Naomba ndugu zangu wengine tusome kwa kumaanisha tutaelewa alichomaanisha.. Eeeh Mwenyezi Mungu, Muumba wa vyote akubaliki na kukutangulia katika kazi za mikono yako na maisha yako yote. Amen

    ReplyDelete
  9. Maneno mazima kabisa,mshika rimoti (FREEMASONS) na agenda yao ya ku control ulimwengu,WOLD NEW ORDER,binaadamu tuamke tumkimbilie ALLAH yeye ndie mwenye kunusuru.

    ReplyDelete
  10. wewe mchangiaji wa mwisho usipotoshe ukweli achana na habari za rais kilichoongelewa hapo kipo wazi kabisa kikwete unamhusisha vp?,nakuomba urudie kusoma hiyo makala ya masoud ili uelewe,jamvi hili si la udaku,tusipende kuponda kila kitu,tafakari kwanza kabla ya kusema chochote.nawakilisha

    ReplyDelete
  11. ankali naona sikuhizi unabana comment zangu nitakuwa sikupokei ughaibuni ukija kwenye vakesheni zako unazolipiwa na CCM na hii pia minyia lakini ujumbe umekufikia.

    ReplyDelete
  12. Michuzi acha kubana comment yangu niliyoitoa mwanzoni. Acha tuelezane ukweli kuhusu mapungufu na mazuri ya imani zetu. Mimi nilimuuliza swali ndg masoud kuwa katika utabiri wake mzuri anafikiri kati ya miungu wawili ninaowajua ni Mungu yupi atakayekosa watu siku zijazo? Manake katika kuishi kwangu nimegundua binadamu tunaabudu miungu wa aina mbili: wa kwanza ni MUNGU WA UPENDO ambaye kwake viumbe wote wana haki sawa bila kujali tofauti walizojiwekea. Ni mungu huyu ndiye anayemtaka mwanamdamu yeyote kutomhukumu mwenzake kifo kwani hukumu hiyo anayo yeye mwenyewe.

    Wa pili ni MUNGU WA FUJO anayeruhusu mtu mmoja au kikundi cha watu kutoa uhai wa watu wengine wasiokuwa na hatia kwa kuwalipua kwenye vyombo vya usafiri, kwenye majengo wanamofanyia kazi au kwenye sehemu za starehe eti kwa sababu ya kutetea dini.

    ReplyDelete
  13. Nyie mnaobisha nendeni mgoogle Rothchilds. Hivi maelewa jinsi uchumi wa Greece ulivyoanguka, na baadae Mkuu wa WB alivyotolewa kwa aibu na sasa wamesema Banks zinafuta 50% ya deni lakini ngoma bado i mbichii!!!

    Pesa, mabenki ndio walioshika remote wakitaka pesa yako wanachukua tu kama walivyobeba za Ghadafi. Mbaya zaidi Ghadafi alitaka kuanzisha benki ya Afrika kama IFM au WB yenye gold currency, na jamaa pesa yao ingekuwa haina thamani. Watu wake wakatiwa maneno wakamuona kama mavi, na hata jinsi walivyoifanya maiti yake ni kama watu wasokuwa na dini wala wasoijua kuna mungu.

    Na bado tunayaona zaidi ya Ghadafi na tutaendelea kuona mengi. Mungu na aniepushe na kizazi changu na kikombe hiki!

    ReplyDelete
  14. hongera kaka. hakika somo lako ni na tafakur ya hali ya juu. ni wanomhofia Allah tu ndo pengine kiurahisi watakuelewa. watakaoshindwa kukuelewa siwezi kuwalaumu lakini pengine yawezekana wamejisahau sana na hata hawajiulizi kwa nini hiki kinakuwa hivi leo badala ya jana au juzi na je kesho na keshokutwa itakuwaje...naungana na walitangulia kwa kumuomba Allah kwa namna yeyote ile atuepushe mbali na hili, naomab ambaye hajaelewa hii maada ajaribu kuirudia tena na tena kwa kutulia huenda akaelewa

    mdau
    suleiman
    loptz@yahoo.co.uk

    masoud hiyo ndo mail yangu kaka unaweza kunirushie chochote siku yoyote inshaallah.

    ReplyDelete
  15. Bwana masoud, anazungumzia mambo ya kusadikika(ficticius) ambayo hayana uwepo(existance) ni kama amepata luya au watu wengine wanasema unaota kwamba huenda kuna kitu cha namna hii, mtu anaweza akafanya juhudi katika maendeleo na asiyapate, wengine wanasema, usipoandikiwa huwezi kufanikiwa, sasa nani anaandika kuhusu viumbe huyo atakuwa muumba wako kama neno hili linaukweli,lakini kusema eti kunawatu wameshika remote control ili wengine wasifikie malengo mmoja mmoja au nchi kwa ujumla hiyo ni very abstract, kwasababu kama hao wameshika remote nawe unawaona kwa nini usiwanyang'anye hiyo remote or why don't you go around them with your Tv. in this case.
    Bwana Masoud, mimi nakuunga mkono kabisa lakini inayoweza kufanya hivyo ni mamlaka ya juu na siyo viumbe walioumbwa na Mungu kama binadamu ungesema some Gods doing this ningekuelewa.hapo napenda nikujulishe tu kwamba,kuna Mungu mkuu na Miungu, hawa miungu ndo wakorofi wanaweza kufanya hivyo I believe.

    ReplyDelete
  16. Masoud, watu umewaacha mbali mno,ila ulichataka kuwafahamisha ni simple kabisa isipokuwa umetumia lugha ndefu bila sababu. jamani ,masoud ana maana kwamba sasa hivi watu wa chini wote wameshaamuka,dunia nzima, angalieni huko Syria, Yemen, Lybia, wall street, walala hoi wanaandamana kutaka haki zao,na ndiyo maana Gadaffi wakamtoa kwenye mtaro wa taka na kumchapa makofi kisha kumuweka risasi la kichwa, Saddam naye vile vile na wengine wengi watafuata, hii ni karne ya vijana na mawasiliano ya papo kwa hapo, internet na face book N.K huko tunakokwenda kutakuwa hakuna binadamu (miungu). all wrong doazi will be put to justice-mwanamume Bush alitamuka hili-sasa tunayaona. Masoud weka wazi,najua wewe ni mwislamu na hukutaka kumtaja Bush.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...