Benki nyingi hapa Sauzi zina huduma ya moja kwa moja (automatic) kukuambia nini kinaendelea katika akaunti yako.
Yaani mara tuu fedha inapoingia kwa akaunti, muda huo huo unapata meseji kwa simu yako kuwa fedha imeingia, na kama imetoka pia wakati huo huo unapata meseji.
Hii ina maana kama umemtuma mtu akakuwekee fedha, atakudanyaje kama aliweka, kumbe hakuweka ?
Pichani ni moja ya meseji iliyoingia baada ya rafiki yangu wa Kisauzi kuwekewa fedha na jamaa yake wa town nyingine. Capitec ni moja ya benki hapa Sauzi.
Na Mdau John.
Sauzi
Kumtembelea BOFYA HAPA



We mleta mada, mara ya mwisho kuja Bongo ilikuwa mwaka gani? Naona unashobokea vitu ambavyo ni vya kawaida sn TZ. Hata hapa Uswazi huduma hiyo ipo siku nyingi tu. Hujapata kusikia kuhusu NMB Mobile ama ile ya sms banking ya CRDB? Zina utaratibu huo huo km wa benki za sauzi!
ReplyDeleteasante sana kwa taarifa yako nzuri ila kwa huko afrika inaonekana ni kitu kipya lkn kwa huku ulaya na marekani hata ukitaka kujua acount yako kama una akaunt bank za huko nyumbani unajua tu kupitia simu yako
ReplyDeletewewe anon wa kwanza unachozungumzia na anachosema mtoa mada ni tofauti. mimi nimejiunga na simu banking ya crdb miaka 2 iliyopita, mpaka leo sijawahi kupata any sms inayonijulisha transactions ninazofanya kwenye account yangu, mshahara wangu unapita huko, kwa hiyo ni account ambayo naitumia sana tu.
ReplyDeletebarclays bank hapa bongo inafanya hivyo mbona siku nyingi wajameni,acheni kushoboka
ReplyDeleteUBA Bank PIA TUNAYO HIYO HUDUMA HAPA TANZANIA.KUANZIA UNAPOFUNGUA AKAUNTI UNAJULISHWA JUU YA AKAUNTI NAMBA YAKO HADI UNAPOFANYA ANY TRANSACTION LAZIMA UPATE SMS KUAMBIWA JUU YA HILO.
ReplyDeleteAsanteni wadau wooooooooooote kwa taarifa wengine tulikuwa hatujui, tuna account katika mabenki lakini hatuna taarifa muhimu kama hizo. Mshukuruni mdau aliyeleta mada hii, kwani kawasaidia kujitangaza nimejua kuwa barclays, UBA nk mnatoa huduma hizo. Msimshambulie tuu mtoa mada. by the way Michuzi inabidi uwe unacharge kwa kujitangaza kwa style hii, kama hivi nimeelimika na natamani kufungua account Baclays sasa wao watapata faida ya mimi kuwa mteja wao na wewe Ankal?? Chukua hatua!!!!!!!!!!
ReplyDeleteKitu kizuri sana! ngona tufuatilie tunaambiwa hata huku kipo basinasi bank zetu zimeendelea.Lakini sisi kama wateja hatujui hatuoni kama bank zetu zimelala? Kweli bank zimshukuru mtoa mada maana amezisaidia kujitangaza!
ReplyDeleteTANZANIA POSTAL BANK HAVE THAT SERVICE AND ITS GOOD
ReplyDelete