Huwezi kutumia internet kwa matumizi ya kawaida bila kutumia Internet browser. Hii ni interface inayotuwezesha kufungua blog, websites na progams nyingine za Internet. Kuna aina sita za Internet browser:· Internet Explorer – Microsoft Inc
· Google Chrome – Google Inc
· Mozilla Firefox – Mozilla Corporation
· Safari – Apple
· Opera – Opera Software
· Netscape – Netscape Communication Corporation
Ili kurahisisha matumizi yake, Internet browser zote zinahifadhi kumbukumbu ya web sites zote ulizotembelea. Zinafanya hivyo kwa sababu kadhaa. Sababu ya kwanza ni kwamba kwa kuhifadhi kumbukumbu hizo huwa inamrahisishia mtumiaji anapotaka kutembelea website hizo hizo hapo baadaye. Hii inapelekea internet experience kuwa faster kwa sababu baadhi ya information imehifadhiwa kwenye komputa yako na sio kwenye server maili kadhaa kutoka ulipo.
Pamoja na kwamba web browser inaokoa muda wako, kuna mswala kadhaa yanayoweza kuleta madhara kwenye komputa yako.
Kawanza kumbuka kwa kuwa wewe umerahisishiwa unapotembelea web sites ulizozea, hali hii inamwezesha mtu mwingine kuziona kumbukumbu hizo zinazohifadhiwa na web browser. Baadhi ya web site ulizotembelea inawezekana information zilizohifadhiwa ni muhimu au za siri (kama mambo ya kiakazi). Mtu mwingine mwenye nia mbaya anaweza kujua kila website uliyotembelea na nini ulichofanya kwenye website hiyo. Kuepusha watu kuona information zako usiache fingerprint unapotumia internet. Unafanya hivyo kwa kufuta (delete) kumbukumbu zote ambazo web browser imazihifadhi.
Unaweza kufuta kumbukumbu hizo kirahisi kabisa kama ifuatavyo:
· Google Chrome: Select “Tools” and choose “Clear Browsing History”
· Safari: Click on the “History” tab in your menu bar. Select “Clear History” located at the bottom of the list.
· Internet Explorer: Select the “Safety” drop down menu at the top right of the screen. Choose “Delete Browsing History.”
· Mozilla Firefox: Click on the “Tools” menu, then select “Clear Recent History.”
Pia kuna njia nyingine unayoweza kutumia web browser bila kuacha fingerprint. Web browser zote zina feature inayokuwezesha kufanya hivyo: Kwa watumiaji wa Internet explore hii inaitwa “In Private”; kwa Mozilla Firefox na Safari hii inaitwa “Private Browsing”; na kwa Google Chrome hii inaitwa “incognito”. Njia hii ni nzuri zaidi hasa kwa wale wanaotumia komputa za public kwa mfano café, shuleni, vyuoni, kazini, n.k.
Kila la kheri


sio kweli kwamba kuna aina 6 ya browsers; zipo nyingi sana labda zaidi ya Ishirini. Ningekuelewa kama ungesema kuna "aina kuu 6" za browser. Kama wewe ni mtumiaji wa Linux au Ubuntu unaelewa ninachosema hapa.
ReplyDeleteLutinwa
Naona mshirika, nia yako ni nzuri ila umejichanganya..in private browser inafaa kama upo nyumbani, kw akompyuta unayoitumia kila siku, maana jama kujua websites zipi unaangalia sio zile kurasa zimetunzwa kweney 'cache' ila cookies ambazo wadau wanajua in real time unafanya nini. kwa hiyo next time ukiingia toka kwa kompyuta hiyo wanajua walete matangazo gani ya biashara, zaidi wanajua uko nchi gani.
ReplyDeletesasa kwa kompyuta za kafe au public places, uko utawaacha waangalie tu ( cookies) ila ukimaliza unataka kufuta hizo kurasa kweney cache.
Inapoafungua email, mfano kweney Google ya kiswahili, angalia upaneda wa kulia utapata matangazo kibaho ya kuhusu kiswahili, ama kjifunza, au Tanzaia, hoteli Bongo, tiketi za ndekege nk, hizi hawazipata ukitoka kweney browser ila unapokua una 'surf'.
endelea kuhelimisha jamii
Kama hamjui Computer msiandike upuuzi hapa mnapotosha tu watu. Usijue vitu nusu nusu halafu ukajifanya mwalimu. Ati mtu anaenda kwenye kozi ya wiki tatu ya computer halafu anajifanya lecturer....!!MDAU-NYC
ReplyDeleteKuwasaidia kuclear history pekeyake haitoshi kama unataka kukata mzizi wa fitina unatakiwa ufanye zaidi mfano kwa watumiaji wa google chrome nenda settings->options->under the hood->clear browsing data hapo kuna vipengele mbalimbali unaweza kutik ili vifutwe kama clear browsing history,clear download history,empty cache,delete cookies and other site and plugin data,clear saved password n.k ukifanya hivyo basi unakuwa umeng'oa mzizi wa fitina kwa sehemu kubwa lakini hata hivyo kila unachokifanya huwa kinabaki kwenye hard disk ya kompyuta yako.
ReplyDelete