Napenda kuwajulisha wananchi na wadau wote kuwa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma Sura 257 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 (The Public Corporations Act, Cap. 257 of R.E. 2002) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jenerali Mstaafu Robert P. Mboma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuanzia tarehe 27 Oktoba 2011 baada ya Bodi iliyokuwepo kumaliza muda wake tarehe 26 Oktoba 2011.

Pamoja na uteuzi huo, Mheshimiwa William M. Ngeleja Waziri wa Nishati na Madini kwa Mamlaka aliyonayo amewateua wakurugenzi wanane wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania kuanzia tarehe 27 Oktoba, 2011.  Walioteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Bodi ni pamoja na:-

1.    Bw. Baruany Elijah A. T. Luhanga
2.    Bw. Ridhiwan Ali Masudi
3.    Bw. Leonard R. Masanja
4.    Bw. Vintan W. Mbiro
5.    Bw. Beatus P. Segeja
6.    Bw. Hassan Ally Mbaruk
7.    Mhe. Victor K. Mwambalaswa (Mb.)
8.    Bw. Abdul Ibrahim Kitula

                                                                     Imetolewa na:
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ushauri kwa Rais Kikwete, mbona vijana wasomi hawapi nafasi kama hizi? Sasa wanasoma tu bila kupata madaraka? Kwani Tanzania damu changa ambazo wenzetu wa Marekani na Ulaya wazitumia, kwa nini sisi tunazidharau? Wazee wale wale tu toka uhuru hadi sasa miaka 5o baada ya uhuru hawawaachii vijana?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...