Lori hili lilikuwa limesimama barabarani tena katika sehemu ambayo hakuna kwa kuegesha magari na huku kukiwa hakuna tahadhali yeyote,hali ambayo inaweza kuleta hatari kubwa iwapo kunakuwa na gari iliyo kwenye mwendo mkali ikitokea kule juu.uzembe wa namna hii unatakiwa kukomeshwa haraka iwezekanavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kusema kweli hilo lori ndio, limepaki kimakosa.Lakini ukiangalia katikati ya barabara kuna misitari ambayo inatoa tahadhari kuwa sehemu hii si salama, endesha kwa uangalifu. Lakini kutokana na madereva wengi kutokuwa na elimu ya kutosha ya sheria za uendeshaji ni vigumu kuona vitu kama hivi, na kweli atakuja kasi kutoka juu, na matokeo yake yanaweza kusababisha ajali na kuwa kosa juu ya kosa!!Serikali imejitahidi sana na alama za barabarani, lakini darasa nalo linahitajika ili zifuatwe.

    ReplyDelete
  2. Too nice country, beautiful landscape, very good road marked in international standards, attractive road shoulders, green grass, natural trees, nice photo BUT the truck driver is just a one big fool, or rather stupid,

    ReplyDelete
  3. Huu mlima kama umekaa wima sana hivi gari linaweza kupanda? Na mdau wa kwanza mbona sioni mistari ya nenda kwa uangalifu. Huku kwetu hiyo mistari inamaanisha unaweza ku-overtake. Kwa mfano anayetokea huko juu mlimani anaweza kulipita gari lililoko mbele yake kama ni kweupe na anayepandisha mstari wake ni solid hivyo hawezi kulipita gari lililoko mbele yake. Na hapa chini ni dash kote kwahiyo pande zote zinaweza overtake. Labda kama ulivyosema ina maana nenda kwa uangalifu kwa sheria za Bongo

    ReplyDelete
  4. Na hiyo barabra kama ulimi kwa upana wake divider ni rangi jamani tembeeni muone watu wanavyo jenga bara bara zao ni vigumu kusikia gari zimegongana uso kwa uso Wananchi tumelala mno hatuji kasor, quality wala udanganyifu

    ReplyDelete
  5. Bara bara zetu ndio chanzo kikubwa cha ajali nchini uzuri wa bara bara sio lami tu hizi za kwetu nyembamba mno ndio utasikia magari yame gongana uso kwa uso

    ReplyDelete
  6. hivi kwani hapo limesimama au linaingia barabarani? sio mnakimbilia tu kurusha shutuma kwa huyo dereva

    ReplyDelete
  7. Wachapwe viboko hadhalani....na kwenda jela....wakitoka jela..wachapwe viboko mbele za wake zao....

    ReplyDelete
  8. Lazma Serekali ianzishe kikosi maalumu cha kunaganlia wavunjaji sheria za usalama Barabarani.
    Tena walipwe vizuri kuepusha Rushwa la sivyo nchi yetu inatia aibu kwa kusababisha ajali zinazo sababishwa na uzembe wa hali ya juu.
    Ajali ndiyo zinachakaza barabara pia pamoja na kupunguza nguvu kazi ya Taifa.
    Pia ,ni muhimu kuwa na sehemu za kuegesha maroli kila baada ya kilometa kadhaa.

    ReplyDelete
  9. ...Mdau wa tatu, hizo alama ni za kimataifa kama unatoka juu, ina maana huruhusiwi kuendesha upande mwingine wa barabara!!..ina maana huwezi ku overtake....Hairuhusiwi hata bongo, kama unavyodai, lakini kama mdau wa kwanza alivyosema, ni darasa la uendeshaji ndio pungufu kwa madereva wengi bongo.Pili, huoni kibao cha tahadhari kwa sababu hiyo tahadhari tayari imewekwa katika barabara, kama huna darasa vitakupita tu.Tatizo lingine si barabara kuwa nyembamba, ila uvunjaji wa sheria ndio mara nyingi zinasababisha ajali za uso kwa uso!!!..mfano hapa Dar, mara ngapi umeona magari yanapita baada ya taa nyekundu kuwaka? au right turn hata kama taa nyekundu inawaka?...ukosefu wa elimu ya uendeshaji inachangia ajali kwa kiasi kikubwa!!!!

    ReplyDelete
  10. Heee...Kaka!!...mdau wa tatu, hiyo alama hapo katikati hauruhusiwi ku overtake, na ni ya kimataifa!! tatizo linakuja mnapozitafsiri mnavyotaka nyinyi!!! una uhakika kwamba inaruhusu ku overtake???..hiyo comment yako inadhihirisha kwa nini mizinga haitopungua bongo!!!....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...