Na Audax Mutiganzi,Bukoba

KAMATI ya usalama barabarani ya mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na askari wa jeshi la polisi wa kikosi cha usalama barabarani itatumia maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari yanayolenga kuwapa uelewa wa namna ya kujiepusha na ajali.

Kwa mujibu wa mwenyekiti ya usalama barabarani wa mkoa wa Kagera Winston Kabantega ni kwamba mafunzo hayo yatatolewa kwa zaidi ya shule 23 za msingi na sekondari zilizoko katika manispaa ya Bukoba.

Kabantega alisema kamati yake imefikia uamzi wa kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi wakati wa maadhimisho hayo ili kuwapa uelewa mkubwa wa matumizi ya barabara hasa wakati wanapotembea kwa miguu.

Alisema wanafunzi ni wadau wakubwa wa barabara kwa kuwa wanatumia barabara kwa muda mwingi, aliendelea kusema mafunzo hayo yatawasaidia namna ya kujiepusha na ajali za barabarani.

Mwenyekiti huyo alisema wanafunzi hao wataelimishwa juu ya alama za barabarani, kanuni na sheria zinazowaongoza wanapokuwa barabarani.

Alisema uelewa mdogo wa wanafunzi walionao juu ya masuala ya matumizi ya barabara ndio unachangia ajali nyingi zinazowakumba wanapokuwa barabarani wakati wakitembea kwa miguu muda wa kwenda au kutoka mashuleni.

Kabantega alisema pia elimu inayotolewa kwa wanafunzi itawajengea uwezo wa kuelewa pia athari zinazotokana na ongezeko la ajali zinazotokea ndani ya jamii, alimaliza kwa kusema ajali znapotokea ndani ya jamii zinadumaza maendeleo kwa kuwa zinachangia kupunguza nguvu kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...