Mafunzo  ya siku mbili ya maadili na Uandishi wa habari za Michezo yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa habari za Michezo nchini TASWA na kushirikisha waandishi wa habari za michezo 40 kutoka mikoa ya Dar es Salaam,Pwani na Morogoro, yameanza leo mkoani Morogoro na kufunguliwa na Mbunge wa Morogoro mjini Abdul-Aziz Abood (wa pili shoto). Pichani Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo nchini TASWA Maulid Kitenge akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayodhaminiwa na Vodacom Tanzania.
 Picha ya Pamoja ya baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa na Mbunge wa Morogoro mjini Abdul-Aziz Abood mara baada ya kufungua mafunzo hayo.
Mmoja ya waendesha mafunzo hayo Mwandishi Mkongwe Said Salim akizungumza jambo na Makamu Mwenyekiti wa TASWA Maulid Kitenge wakati wa mapumziko ya chai.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...