Mabondia Francis Miyayusho (kushoto) na Mbwana Matumla wakitunishiana misuri leo baada ya kupima katika ukumbi wa Amana Dar es salaam kwa ajili ya mpambano wao kesho.

Na Mwandishi Wetu.

Mabondia Mbwana Matumla 'Golden Boy' na Francis Miyayusho 'Chichi Mawe' leo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa Ubingwa utakaofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es salaam kesho jumapili OKTOBA 30.

wakizungumza wachezaji hawo kwa wakati tofauti baada ya kupima wamesema wapo tayari kuonesha mchezo mzuri wa ngumi na kuwapa raha zisizo na kifani kwa sababu akuna kisingizio chochote kile kwa kua tumejiandaa vya kutosha

Licha ya mabondia hao kupima uzito pia wamepima vipimo mbalimbali hususani Ukimwi, Mkojo kwa ajili ya kuangalia kama mabondia hao kama wanatumia madawa ya kuongeza nguvu.

Pambano hilo kubwa litakuwa la 12 la uzito wa Bantam, ambapo kabla ya mpambano kutakua na mapambano mengine ya utangulizi.

Mapambano hayo ya kati ya Juma Fundi na Fadhili Majia, Mohamed Matumla na Ramadhani Mashudu, Issa Sewe atazidunda na Ramadhani Shauli wakati kwa upande wa ngumi za wanawake Asha Nzowa (Asha Ngedere) atazichapa na Salma Kihobwa (mwajuma Ndalandefu)

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinbu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, MOhamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. katafuteni kazi za kubeba maboks acheni michezo ya kuchapana mtakuja kutoana roho bure msosi wenyewe finyu

    ReplyDelete
  2. Hawa Mbona kila siku wanatunishaana Misuri tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...