Mechi namba 63 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Villa Squad na Moro United iliyochezwa Oktoba 1 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam imeingiza sh. 396,000.
Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 132 ambapo kiingilio kilikuwa sh. 3,000 kwa mzunguko na sh. 10,000 kwa VIP. Hakuna tiketi hata moja iliyouzwa kwa VIP wakati mzunguko ziliuzwa tiketi 132.
Baada ya kuondoa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 60,400, fedha zilizobaki zilikuwa sh. 335.600. Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 20,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 20,000.
Posho ya kujikimu kwa kamishna sh. 40,000 na mwamuzi wa akiba sh. 30,000. Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 9,240 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata sh. 7,920. Usafi na ulinzi zililipwa sh. 199,200.
Kutokana na mapato yaliyoingia; uwanja, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) hawakupata mgawo wowote. Pia TFF ililazimika kulipa gharama nyingine za mchezo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari


Hayo mapato ni kwa US Dollar au ni Tz shilings? kama ni dollar sio mbaya kama ni shilingi ya tanzania inabidi mjifunze namna ya kufanya promotions ili kukuza kipato! Namna hii mtaua sports nchini! Hapo wachezaji hawakulipwa kitu! sasa wataishije?
ReplyDeleteAnony wa Sun Oct 02, 07:17:00, inaelekea umekilimbilia kusoma kichwa cha habari wakati tarakimu zote uliacha kichwa cha habari zinaonesha ni shilingi. Hizo ni hela zetu za madafu mdau na hilo ndio soka letu
ReplyDeletekichwa cha hahabi hakina shilingi,hili pato nii sawa na 185 pounds.kwa mtu kuuliza hili swali unatakiwa ujue ni (rhetorical question)elewa hapo.pili ameonesha KAMA NI Shs nini la kufanya (mf:promotion)binafsi nampa mchangiaje wa kwanza,maneno kidogo ujumbe mie...
ReplyDeleteNatafuta timu ya ligi kuu ya kununua huko bongo, nina pound 1000 nimesave zinatosha. Mdau
ReplyDelete