Meli ya Kijeshi kutoka Afrika Kusini SAS DRAKENSBERG ikiwa imetia nanga katika bandari ya Dar es salaam kwa ajili ya mazoezi ya kijeshi ya nchi za SADC ikiwa na wanajeshi wa Kenya,Msumbiji,Tanzania,Zimbabwe na wenyewe Afrika Kusini.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. ANKAL LEO NINGELIPENDA NIKUJUZE KIDOGO KATIKA UFASAA WA HIVI VYOMBO VYA BAHARINI AU KATIKA MAZIWA KWA MAANA YA MAJI BARIDI KAWAIDA CHOMBO AU MANUARI KAMA HIYO HAPO ILIPO IMEFUNGA GATINI AU KWA LUGHA ZA WENZETU IPO ALONGSIDE SIO KUTIA NANGA KWA UFAFANUZI ZAIDI NANGA NI CHOMBO MAARUMU CHA KUZUIA MELI NDANI YA MAJI IWEZE KUWA SEHEMU MOJA AU KUZUNGUKA SEHEMU MOJA NA HUTOSWA NDANI YA MAJI NA INAKUWA NA CHAIN MAARUMU YA UREFU KADHAA KUTOKANA KINA CHA HIYO SEHEMU INADONDOSHWA NDANI YA MAJI KWA KUIZUIA MELI ASIHAME SEHEMU HIYO KWA MFANO WA WAZI KABISA UKIFIKA HAPO POSTA YA ZAMANI UTAZIONA MELI ZIPO NDANI BAHARI KATI YA FERI NA HAPO NDANI BANDALINI HIZO NDIZO ZILIZOTIA NANGA IKISHAKAA KATIKA UKUTA WA BANDALI HIYO INAKUWA GATINI AU ALONGSIDE NA ZILE AMBAZO HUONEKANA NJE YA BAHARI HASA UKIWA MAENEO YA FERI AU KULE NYUMA YA IKURU UTAZIKUTA, ZILE ZIKO NANGANI PIA NIMEPENDA NIKUJUZE MAANA HUWA NAONA WAANDISHI WENGI MELI IKIWA GATINI WANAANDIKA IPO NANGANI NI HAYO WAKO MDAU richie wa ughaibuni

    ReplyDelete
  2. Ni vizuri kujuvyana kiswahili sahihi au fasaha. Hongera mdau wa ughaibuni kwa kumuelimisha kiwahili fasaha mwandishi.

    Ila hata nawe yafaa kuelimishwa usahihi wa kiswahili kwavilile yaonekana kama ni mkuria fulani hivi wa ughaibuni.
    "chain maarumu" usahihi wake ni mnyororo maalumu.

    "meli zipo ndani ya bahari" usahihi wake meli zipo baharini, zikiwepo ndani ya bahari zitakuwa zimezama hizo kama nanga inavyotoswa ndani ya maji.

    "Bandali" usahihi wake ni bandari.

    "Ikuru" usahihi wake ni Ikulu.

    Natumai nimekujuvya vya kutosha mdau wa ughaibuni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...