Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu akitazama aina mbali mbali za maharage na kunde kunde katika soko la Tandale alipotembelea soko hilo kujionea hali ya soko na upatikanaji wa vyakula na bei.
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu akitazama aina mbali mbali za mboga mboga katika soko la Tandale.
 Wateja wa mboga mboga wakiwemo wageni kama walivyokutwa spokoni Tandale wakijipatia bidhaa mbali mbali za vyakula sokoni hapo.

Wafanyabiashara wa nguo za mitumba katika soko la Tandale wakizungumza na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe lazaro Nyalandu sokoni hapo. Wamemuomba Mh Nyalandu kuwasaidia kuboresha mazingira ya soko hilo ili kuvutia wateja zaidi.

UZENI BIDHAA KWA BEI HALALI.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu, amewataka wafanyabiashara na mamlaka husika kushirikiana ili kuhakikisha kuwa  bidhaa katika masoko hazuizwi kwa bei aghali kuliko bei iliyopangwa katika soko.
Mh Nyalandu ametoa wito huo  Jijini Dar es salaam, mara baada ya ziara yake ya ghafla katika soko la Tandale ambalo ni miongoni mwa masoko yanayopokea kiasi kikubwa cha chakula kutoka kwa wakulima kote nchini.

Katika ziara yake hiyo, Mhe Nyalandu amewataka wafanyabiashara kuwa waungwana na wazalendo kwa kuuza bidhaa mbali mbali hasa vyakula kwa bei nafuu ili wananchi wenye vipato vya hali chini waweze kumudu.

Hali ya chakula nchini ni nzuri, nafaka, mbogamboga na matunda vinapatikana kwa wingi. Wakulima wanawauzia wafanyabiashara kwa bei nzuri na nafuu, natumia nafasi hii kuwaomba nyinyi wafanyabiashara kuwa wazalendo, tuwajali wateja wetu kwa kuwauzia bidhaa hizi kwa bei watakayoimudu, mpate faida kidogo na wenzenu wapate chakula na mahitaji mengine kwa bei nafuu.

Mhe Nyalandu pia ameutaka uongozi wa soko hilo kubuni mbinu za kisasa za kuliboresha soko hilo liweze kuvutia wateja zaidi wa ndani na nje ya nchi, kuimarisha hali ya usafina kuzingatia kanuni za afya ili kuwalinda walaji dhidi ya magonjwa yanayoweza kusababishwa na uchafu



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...