Mjukuu wa Madiba ambaye aliwahi kushiriki Big Brother -3 THAMI PRUSENT amefika nchini  ambapo alihojiwa katika kipindi cha Jambo cha TBC1 asubuhi Septemba 30, 2011 na Marin Hassan. Yuko katika safari kutoka Capetown kwenda Cairo Masri for Free akichangisha fedha kuwasaidia wahanga wa njaa nchini Somalia. 

Alimuomba msaada wa tiketi ya treni kutoka Dar kwenda Kigoma Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu ambaye aliafiki ombi lake. Jana Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Dk Richard Kailembo alimkabidhi rasmi tiketi ya daraja la kwanza kutoka Dar kwenda Kigoma na zawadi nyingine! 

Kwa hiyo Thami ameondoka na treni yetu ya abiria saa 11 jioni kwenda Kigoma ambako anatarajiwa kuwasili leo Oktoba 06,2011 Alhamis asubuhi ambako atasafiri kwa boti kuvuka Ziwa Tanganyika kwenda Bujumbura Burundi na baadae Kigali Rwanda ikiwa ni mwendelezo wa safari yake ya Kampeni kuelekea jijini Kairo Misri ( au Masri kwa sisi Waungwana!) ambapo itakuwa tamati ya safari yake hiyo!
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Dk Richard Kailembo akimkabidhi fulana na kofia na vipeperushi kijana Thami Prusent zenye nembo na kauli mbiyu ya TRL kama kumbukumbu ya kutembelea Makao Makuu ya TRL.
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Dk Richard Kailembo akimkabidhi mkoba wa zawadi pamoja na  tiketi ya daraja la kwanza Thami Prusent ya safari kutoka Dar hadi Kigoma.
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Dk Richard Kailembo akimtakia  Thami Prusent safari njem kabla ya kuanza  safari kutoka Dar hadi Kigoma.

Meneja wa Uhusiano wa TRL Mdau Midladjy Maez akimuaga Mdau Thami Prusent akiwa tayari ndani ya treni kuelekea Kigoma hapo  Oktoba 04, 2011 katika Stesheni ya Reli ya Kati ya Dar es Salaam.

 

Kaimu Mkuu wa Masoko wa TRL Bw Hassan Shaaban akimuaga Thami

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Duh, kama hilo daraja la kwanza ni chafu namna hiyo je la tatu litakuwaje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...