Mlinzi akiwa katika tundu lake akilinda magari katika maegesho ya magari ya Mlimani City jijini Dar es salaam kudhibiti wizi wa magari, ikiwa ni kujaribu kumaliza malalamiko yaliyokithiri mahali hapo kwa siku nyingi ambapo wanaokwenda kufanya shopping wamekuwa wakiibiwa magari ama vifaa vya magari na mali zao kila kukicha.
Walinzi wakibadilishana mawazo wakiwa katika lindo ambalo inasemekana kiasi limesaidia kupunguza udokozi wa mali na wizi wa magari Mlimani City. Hata hivyo kuna minon'gono na alama za kujiuliza kwamba badala ya kutumia kamera maalumu (CCTV) kwa nini uongozi uweke CCTV chapa mtu ikizingatiwa ukubwa wa eneo pamoja na udhaifu wa kawaida wa kibindamu unaoweza kuwakumba walinzi hao, ikiwa ni pamoja na kwenda kujisaidia ama kupiga stori kama hivyo hapo juu. Bongo Tambarare.....
MAREHEMU BONGO
ReplyDeleteSi niliwaambia wabongo ni watu wa mzaha ktk hata mambo ya hatari. Waambieni makaburu wanunue mitambo ya kisasa na hayo makampuni ya ulinzi yafunzwe kuitumia. Hapo huyo mlinzi natumaini anamweleza mwenzie dili la meshen,....unabisha?
ReplyDeleteUNAJUA BAADHI YA WAAFRIKA NI WAPUMBAVU SANA...DAA IMENIUMA SANA,YAANI HATA KITU KIDOGO KINAWASHINDA...HIVI TUNA MATATIZO GANI?HUU NI ULOFA WA HALI YA JUU...HIVI KATIKA UONGOZI WAO WOTE HAKUNA MTU AMBAYE AMEJERIBU KUFIKIRIA ZAIDI YA KUWEKA HIKO KITUNDU CHA NDEGE...POLE YENU WAAFRIKA NA SIRUDI NG'OO AFRICA.
ReplyDeleteSIAMINI KAMA KAMPUNI ZOTE ZILIZOPANGA HAPO MLIMANI KWA PAMOJA BADO ZIKO KWENYE UJIMA WAPENI SEMINA NA PICHA ZA WENZETU WANAFANYAJE KWENYE BIASHARA ZAO
ReplyDeleteHAO WALINZI NDIO VIBAKA WAKUBWA WAO NDIO SHINA LA MESHENI MGAO BAADAE
ReplyDeletehahaa.. Tatizo la bongo CCTV huyo huyo ndiyo anachora ramani ya ukwapuzi.. Kama ilivyo filosofi iliyozoeleka kuwa "Utakula Kazini"
ReplyDeleteTatizo hapo ni kama vile kukaa shamba ukiamia ndege, yaani unapiga kelele ili waruke wasile mpunga, au kukaa karibu na vifaranga vya kuku Dar ukifukuza kunguru. Mimi binafsi naona the only way ya kudhibiti vibaka ni kuhakikisha Mlimali City wanajenga parking ya Kisasa kama yenye ghorofa kuanzia moja kwenda juu na huko ndiyo waweke CCTV pia kuwe na Gate linalodhibitiwa. Maana yake ni kwamba hataenda mtu bila kuwa na gari na wacharge at least TZS 300 kwa kupark. Kama vibaka wataenda na gari juu, hapo ndipo CCTV itakuwa na maana. Kwani mnawaangalia wanavyofanya hamuwashtui, wakianza kuondoka wakifika getini mnawatia mbaroni Kwishney.
ReplyDeleteIla hapo Open space wakwapuaji hawatakosekana maana mtu anajua akiisha kwapua tu anatoka nduki hata kama mtamnasa kwenye CCTV mnajua anakokaa?. Kama Polisi wameshindwa mpaka kumkamata aliyewapiga risasi kina CHIGUMBI wa Mahenge japo walikuwa na taarifa zake kama muajiriwa je mateja wa mtaani?
Na ninyi tumieni akili. Sasa wakiweka CCTV kwani mna database gani ya kuwatambua hao watu? Itachukua muda gani kuwa-identify na kuwa-locate watu ambao wengine wanalala chini ya madaraja na hawana hata makazi au address. Hiyo ndo solution iliyopo kulingana na uwezo uliopo. Ni kama kumkamata mtu halafu uchukue fingerprints wakati huna fingerprint database....kwani akifanya uhalifu mwingine utawezaje kufanya comparison kumtambua? Ninyi kazi kulaumu tu wakati hamna solution. Angalau wameweza kupunguza vibaka. MDAU_NYC
ReplyDeleteWEWE MDAU WA NYC NILIJUA UNA AKILI KWA KUKAA MAREKANI KUMBE NA WEWE NI MPUMBAVU,KWA TAARIFA YAKO BONGO KUNA DATABASE YA WAHALIFU TATIZO WANAKUWA NA MZAHA SANA NA KUCHUKULIA MAMBO KIENYEJI NA ISITOSHE HIVYO POLISI WENYEWE HAWANA E-MAIL ADDRESS UNATEGEMEA ATATUMIA COMPUTER..ACHANA NA HAYO CCTV INAWEZA KUWEKA NA KUKAWA NA WALINZI GETINI MTU AKIKWAPUA ANAONEKANA KIURAHISI NA KUTAITIWA GETINI,CCTV TUNAYOTAKA IWEKWE NI YA KULINDA MAGARI HAPO KWA HAPO SIO MTU AIBE THEN NDIO TUANZE KUANGALIA CCTV INGAWA INAWEZA KUTUMIKA KWA MTINDO HUO....DAA NGUMU SANA KUELIMISHA WAAAFRICA.
ReplyDeleteKwa mazingira na infrastructure za Tanzania combination ya CCTV na physical guarding ni muafaka kabisa. Kumbuka wezi wanambinu nyingi na immediate response ni muhimu. Likewise, vibaka kwa kawaida wakijua kuna physical guarding si rahisi kuiba kama vile ambavyo zikiwepo kamera. Kamaera zitumike na physical guarding iwepo. Hata katika nchi kubwa kama US kwenye parking lots zipo CCTV kamera na pia physical guards wanakuwepo muda wote, si jambo geni.
ReplyDeleteHiyo CCTV chap mtu itamjuaje mwenye gari?
ReplyDeletewaosha vinywa bwana, sasa cctv itasaidia nini? mimi nishawahi kupewa mchongo Game, attendant anakwambia sogea kona ya kwenye aisle maana hapo camera haikuoni, anachukua cut yake halafu yeye anakuwa keshapiga dili na cashier, cashier anascan kitu kwa bei less halafu anakula sahani moja na mlinzi anaegonga risiti mlangoni. mchongo wote huo supervisor anaujua. Sasa wewe kibaka anaetumia 30 secs ukimuona kwenye CCTV itasaidia nini? atleast hapo jamaa akiona kibaka tu ni kutoka nae nduki.
ReplyDeleteHiyo cctv si itavalishwa nguo, then watu wanachakachua.
ReplyDelete