Salam za kazi  kaka Michuzi.

pole na kazi na hongera kwa kuhabarisha jammi, kaka mimi ninashida moja ninaishi ughaibuni na ninashida na contacts 
yaani namba za simu pamoja na email za ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria

nilikwenda google kutafuta contacts zao kwa bahati mbaya namba zao za simu zote walizoweka mitandaoni hazifanyi kazi
so nashindwa kuelewa namba sahihi ni ipi hata email hazijibiwi. nitafurahi sana ukinisaidia na contacts hizo haraka iwezekanyo.

ahsante

Mama Z

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mama Z, hawa watu walishahama Lagos wako Abuja. Unfortunately it has been yeras tangu waame lakini bado wanaandika address ya Lagos. Tembelea website ya foreign affairs then utapata details waliko

    ReplyDelete
  2. Piga namba +255 784 215474 afisa wa Ministry of Foreign Affairs Tanzania atakusaidia hiyo information.

    ReplyDelete
  3. BORA UMESEMA MAMA,SISI WAAFRICA SIJUI TUNA AKILI GANI HILO TATIZO SIO TU LA NIGERIA HATA NCHI NYINGINE PIA SIO TU HILO UTASHANGAA UBALOZI MKUBWA WA TANZANIA WA NCHI KAMA UK HAWANA HUDUMA NZURI INAYOELEWEKA,NIMESHAGAA KUONA FORM YA KUOMBEA KUNA SEHEMU IMEANDIKWA KWA MKONO HAALAFU IKAWEKWA MTANDAONI..NI VITU VIDOGO SANA ILA VINATUTIA AIBU KUBWA SANA...TATIZO LA SISI WATU WEUSI TUNAPEANA PEANA KAZI TU HATA KAMA MTU HANA UJUZI NAYO KWA KWELI SIWEZI KUAMINI UBALOZI KAMA WA WATNZANIA UNAWEKA FORM IMEANDIKWA KWA MKONO...WAPENI KAZI WAJUZI JAMANI CHEKI HII FORM HAPO KWENYE KISANDUKU CHA PICHA http://tanzaniahighcommission.co.uk/images/stories/tanzania_visa.pdf

    ReplyDelete
  4. Ninaunga mkono maoni yaliyotolewa na ndugu zangu hapa. Balozi zetu ziko nyuma sana kwani maofisa wengi hawana taaluma zinazotakiwa katika ulimwengu wa sasa. Tatizo labda ni suala la kuajiri watu kutokana na kujuana badala ya kuangalia utaalamu. Miaka michache hapo nyuma nilipata nafasi ya kuenda ubalozini kwetu Washington D.C. na ilikuwa ni aibu kubwa sana. Baada ya kupewa saa ya kuja, nilifika ubalozini mapema kabla ya saa yangu lakini nilikuja kuonana na ofisa wangu baada ya masaa matano. Wakati huo wote watu wanijivuta vuta tu na kupiga hadithi zisizohusiana na kazi. Nilipata pia bahati ya kusikia jinsi maofisa wanavyojibu kwa kiburi na dharau watu ambao walikuwa wakitaka kupata visa za kuja kutembea Tanzania. Ni lazima kutambua kwamba wageni hao wanapokuja kutembea kwetu huwa wanaleta fedha za kigeni na pia husaidia kutangaza nchi yetu, kwahiyo inatakiwa kuwaonyesha ukarimu wetu na kuwakaribisha vizuri.
    Ninaandika maoni haya sio kwa nia mbaya, ila tu ni kuwa wazi ili tuweze kufanya mabadiliko yenye lengo la kuleta maendeleo. Kwa mfano, fomu ambazo ziko kwenye tovuti za bazlozi zetu ni rahisi sana kuzifanya kuweza kujazwa kwa computer badala ya kuandika kwa mkono na kutuma kwa posta, hii itarahisisha kazi sana na kufanya mambo yaende upesi zaidi.

    Mungu ibariki nchi yetu.

    ReplyDelete
  5. anony namba 2 ahsante kwa msaada wako nitawasiliana nao. anony namba 1 wa 09.03am ubalozi wameandika adress zao mbili yaani ya lagos pamoja na abuja pamoja na namba za simu, lakini zote hazifanyi kazi nikipiga naambiwa nimekosea. so nilishindwa kuelewa ofisi zao ziko wapi.

    Mama Z

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...