Habari kaka Michuzi. 

Naomba unisaidie kutoa hii habari huenda nikafanikiwa.Kuna bint anaitwa REGINA FUTE ametoka Njombe jana kuja Dar. Nilitakiwa nimpokee mimi.Bahati mbaya nilipofika  Ubungo sikumkuta.

Nilimsaka mpaka sa 4 usiku bila mafanikio.na watu wengine ambao ni wafanya kazi wa Ubungo station walinisaidia kumtafuta bila mafanikio,wakati tunamtafuta kuna waliotujibu kwamba waliomuona mida ya sa11jioni akiwa anazungukazunguka mdada wa aina hiyo.so nilikua naomba kwa mwenye kumuona atujulishe tafadhali.

Anaitwa REGINA FUTE,AMETOKA NJOMBE NA BUS LUWIZO LILILOINGIA JANA TAREHE 4OCT,BINTI HUYO ALIVAA GAUNI JEKUNDU.

ASANTE SANA KAKA MICHUZI.

0787 472425

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Pole sana ndugu, ila naomba utoe ufafanuzi zaidi kuhusu huyu binti ili
    iwe rahisi kumjua kwa macho.Nakushauri ufahamishe umri wake, urefu,rangi ya ngozi, na ana mwili wa aina gani i.e. kama mwembamba au mnene n.k. Vielezo hivi vitasaidia zaidi kutambulika kwa binti huyu kwa wasiomfahamu. Bandika picha yake pia, kama unayo. Kila la kheri.

    ReplyDelete
  2. Mlitakiwa mumpatie namba zenu za simu kabla hajaondoka Njombe, acheni mambo ya kiswahili. Pia na anwani zenu. Kiswahili swahili hakifai mdada wa watu sasa ameshahifadhiwa bure!!

    ReplyDelete
  3. Mmezidi kurudisha nyuma maendeleo ya mkoa wetu wa Iringa kwa kuufanya kuwa source kubwa ya mahousegirl, hamchokiiiiiiiiiii! tunahitaji kuona wanairinga nao wanajivunia kuwa na wanawake wasomi as compared to other regions.

    ReplyDelete
  4. Anony wa kwanza unajifanya hujui jamani! Urefu, rangi, picha na umri atavijuaje wakati yeye alipewa tu rangi ya gauni ndo ilikuwa ID ya kumpokea ubungo tayari kuja kupiga mzigo home?... Kwa taarifa kuna watu wanakaa pale kituo cha mabasi ubungo kusubiria magari ya iringa, morogoro,mafinga, njombe tanga na singida, wakiona anashuka binti anashangaa shangaa tu kwao ni dili, wanaenda kumuuza kwa wanaotafuta ma-housegirls. Iringa muwe kama mkoa wa Kilimanjaro ma-binti wote lazima waende shule,...lazima.Pole mdau

    ReplyDelete
  5. Kissa Anyigulile: kissaanyigulile@gmail.comOctober 06, 2011

    Well, kwa mtazamo wa wazi unaonekana wewe ndio mzembe.

    Kwa sababu in the face of it, huyo binti anaonekana hajawahi kusafiri nje ya makazi yao, na wewe ukapewa kila details including basi atakalopanda na linaondoka saa ngapi.

    Uzembe mwingine, jambo hili hujasema kama umeripoti Polisi, na pale pale Ubungo kuna kituo cha Polisi. Fanya hima Polisi wafahamishwe, short of that itaonekana hii ilikuwa dili yako.

    ReplyDelete
  6. naona ameboa saana.yani uzembe kama huo hamna cha kumsaidia zaidi tumuifadhi polisi huyo mdau.ataanza kusingizia foleni ooh sababu zilizo nje ya uwezo wake yani ubabaishaji wa kipuuzi

    ReplyDelete
  7. Yaani simu tulizonazo ni za kazi gani? watu mnabeba simu mbili au zenye line mbili za nini kama haziwezi kuwa kitendea kazi. saa hizi mtoto wa watu keshahifadhiwa au kaziniwa, ni aibu sana kwa uzembe kama huu kutokea katika enzi hii ya sayansi na teknologia...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...