Mtoto Sesilia alipowasili nchini India.
Mtoto Sesilia Edward, mwenye umri wa miaka 14 ambaye alisafirishwa kwenda nchini India, katika hospitali ya Fortis iliyopo New Delhi, tarehe 27 septemba mwaka huu, kwa ajili ya matibabu ya moyo, amewasili salama nchini.
Baada ya kupokelewa alipofika nchini India, Sesilia alianza kufanyiwa uchunguzi wa kina na kujulikana kuwa chemba ya juu ya kulia ya moyo wake, imekuwa kubwa kupita kawaida, huku chemba ya chini ya kulia ikiwa ni ndogo kupita inavyotakiwa kuwa, jambo lililopelekea uvujaji katika valvu iitwayo Tricuspid pamoja na kuonekana kwa kimiminika (maji maji) katika tumbo pamoja na mapafu.
Tatizo kama hili lililomkumba Sesilia, liitwalo kwa jina la kitaalamu kama Endomyocardical Fibrosis, hutokea mara chache. Taarifa za madaktari nchini India, zinaeleza kuwa hatua ya kiafya aliyofikia Sesilia katika tatizo hili ni mbaya, hivyo imepelekea kushindwa kutibika kwa ugonjwa huu hivyo atahitaji uangalizi mkubwa kwa kutumia dawa na sio kwa upasuaji wowote ule wa moyo.
Kwa dawa ambazo Sesilia ameanza kutumia mpaka sasa, ameweza kupungua kwa kilogramu tano, anajisikia nafuu zaidi, na afya yake inaimarika. Ugonjwa kama wa Sesilia umesharipotiwa kutokea kwa watoto katika maeneo ya Zanzibar, Pemba, kisarawe Tanzania na Kerala- kusini mwa India.
Dokta Srah Matemu kutoka Hospitali ya Regency amesema kuwa watoto zaidi ya asilimia 20% wanaofanyiwa upasuaji katika hali kama ya Sesilia huwa hawaponi na hivyo madaktari wa hopitali ya Fortis waliamua kutomfanyia operesheni hiyo.
Aidha, tatizo hili limehusishwa na ulaji uliopitiliza wa mihogo yenye sumu iitwayo Cyanide inayopelekea kuvuja na mishipa kusikotakiwa na kudhoofu katika mishipa ya moyo. Katika miaka mitano iliyopita,Sesilia alikuwa akitumia mlo wa muhogo mara tatu kwa siku, amekiri katika kipindi hicho chote, ni mara chache sana amekuwa akila vyakula vingine kama uji,ugali,au wali .
(Sesilia ni mzaliwa wa Kisarawe na amesihi kijijini hapo kwa miaka takribani 13).
Sesilia ataendelea na matibabu na uangalizi zaidi katika hospitali aliyokuwa akitibiwa awali, hospitali ya taifa Muhimbili, huku hospitali ya Regency ikijitolea kumsaidia matibabu ya kupunguza maji na dawa mbalimbali kwa garama nafuu.
Ili kuepuka kutokea kwa tatizo kama hili kwa watoto wengine, Wazazi wanashauriwa kuwa waangalifu katika kupanga milo ya watoto.Uzidishaji wa chakula cha aina moja unaweza kuleta madhara kwa afya ya mtoto kama madhara ya mihogo.
Pia kipindi wanapoona watoto wao hawako sawa kiafya, wawahi hospitali kwa ajili ya matibabu ili kuepuka kukomaa kwa tatizo kunakoweza kupelekea ugonjwa kutotibika. (Dr. Sarah Matemu)
Kipindi cha Mimi na Tanzania, kinatanguliza shukrani zake za dhati kwa timu nzima ya Africa Media Group, iliyoshiriki kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha zoezi la uhamasishaji wa uchangiaji wa pesa kwa ajili ya safari na matibabu ya Sesilia ambayo yamefanyika nchini India.
Pia shukrani ziifikie hospitali ya Fortis Escorts Heart Institute, ambao ilijitolea kwa kupunguza bei ya matibabu ya Sesilia, bila ya kuisahau hospitali ya Regency Dar es Salaam, chini ya uongozi wa Dk. Kanabar kwa kumuandaa Sesilia kimatibabu kwa mda wa wiki moja kabla ya kumsafirisha India kwa ikiwa ni pamoja na daktari kutoka nchini aliyewasindikiza, aitwaye Dk. Ali Amour kutoka hospitali ya Mnazi mmoja.
Shukrani pia zinatangulizwa kwa uongozi mzima wa Lions Club, kwa kufanikisha kwa kuandaa mipango ya matibabu yote ya Sesilia na hospitali, nchini India ambayo yalifanyika kwa bei ya chini kuliko ambavyo hata raia wa India angeweza kutibiwa.
Zaidi ya yote, Mimi na Tanzania inapenda kuwashukuru kwa hali na mali watanzania wote walioguswa na mtoto Sesilia, na kujitokeza kwa kumsaidia kifedha, mavazi na hata kwa sala ikiwa ni pamoja na mahitaji mengine yoyote binti huyu aliyokuwa akihitaji.Moyo wa upendo na huruma mlioonyesha kwa mtoto huyu ni zawadi isiyosahaulika katika maisha yake na wanaomzunguka.
Tusiache kuwasaidia na kubadilisha maisha ya ndugu zetu wahitaji kama hawa. Shukrani!
Usiache kutizam kipindi cam Mimi na Tanzania Jumapili tarehe 22 Oktoba, saa 1:30 jioni – Chanel Ten, kumsikia Dokta Sarah akielezea nini Hatima ya Mtoto Sesilia.
Vyomba vya Habari Tanzania, tumejaribu, tumeweza na yaliyotokea kwa mtoto Sesilia ni kazi ya Mungu.
Fedha zilizobaki zitahifadhiwa katika account ya Mlezi wake chini ya uangalizi ili kumsaidi motto Sesilia kupata matumizi muhimu kama Dawa, kitanda kizuri kumsaidia Mgongo, Kiti maalum cha kukalia na chakula chake ambachohutayarishwa tofauti na vyakula tunavyokula.
Hoyce Temu
Mtayarishaji an Mtangzaji
Mimi na Tanzania
Email: hoyycet@gmail.com
Tovuti: www.miminatanzania.co.tz
Mtoto Sesilia akiongozwa na Madaktari wa Hospital hiyo.
Mtoto Sesilia akipata chakula.
Jamani kwa maoni yangu tu, kwa nini India tu kuna sehemu nyingi kama ujerumani jamani ambaye naamini huyu bi mdogo angetibiwa jamani, huko india wao wenyewe hawajiwezi wahindi. kama msaada unapatikana kwa nini asipelekwe sehemu kama hizo?
ReplyDeleteMwenyezi Mungu akusaiedi Cecilia upone upesi, pole sana na mateso unayo pata
ReplyDeletetafadhali michuzi badilisha hiyo heading hapo,eti karudi bila matumaini ya kuwa mwalim manake nini,ni kwamba atapona na atakuwa mwalimu tena profesa kabisa.
ReplyDeleteJamani Watanzania tuzingatie lishe bora ya afya.
ReplyDeleteLishe duni hufupisha maisha na kuleta matatizo na mateso yasiyo na lazima.
Tuzingatie balance diet kila siku. Ni heri kukosa kuvaa vizuri lakini kumudu balance diet, maana bila hiyo maisha hayana maana.
Hivi lile somo la Sayansi kimu bado lipo mashuleni???
Mtoto wetu pole sana. Mungu atakusaidia utapata nafuu na kuendeleea na shughuli zako za kimaisha, Inshalaah. Ila sikubaliani na wale wanaotaja mara India mara Ujerumani ikiwezekana South Afrika kwa ajili ya matibabu ya Watanzania.
ReplyDeleteMbona mnaganga njaa tu kila siku???? ziko wapi fikira za LONG-TERM intervations kwa ajili ya matibabu si ya moyo tu na mengineyo kwa watanzania.
Madaktari, Madaktari bingwa, na Maprofessa wa kitanzania tunao, Hospitali bingwa tunazo kama nne hivi hapo bongo,
1)Je mnataka kuniambia shida iliyopo ni vitendea kazi tuu??
2)je mnataka kuniambia kuwa Madaktari wetu wana uwezo wa juu wa kimataifa wa kuyakabili matatizo yanayoelekea nchi za nje??
3)Je hatuna junior doctors ambao wanaweza kutayarishwa hivi sasa kwa ajili ya hapo baadaye??
4)Where is our mission for Tanzanians wellbeing.
5)Tusikae na kuwalaumu viongozi in and out, day after days kwa kila jambo, nafikiri mambo mengine yanatakiwa yatokane na wataalamu wenyewe. Wabongo hatuna mwamko, kila tukifanyacho tunategemea malipo ya papo kwa papo, that is very wrong to my mind. Tunakaa tukijisifia kila siku Medical school zetu ni za kimataifa, mataifa yepi? yale ya Tandale au?
Tunatakiwa tubadilishe muelekeo wa fikira zetu, tumezidi mno kuwa tegemezi kwa kila fani. Mabadiliko, Is not always about money, is normally about mission, ideas and motivation to do things independently. Go on Wabongo!!!! Come ON!!!! Madaktari na hasa madaktari bingwa mnajidhalilisha kwa kukaa kimiya, kama mwaweza, semeni twaweza ila........ kuliko kukaa kimiya. Watanzania hatutawaelewa, hatutakuwa na imani na ninyi tunapokuja kwenu hata kwa Malaria na tumbo kuuma.
Insha'Allah Sesilia Atapona kwa uwezo wake Mola,,kwani wote tushirikiane kumuombea kwa Mungu hakuna kinachoshindikana,,,Mimi ninavyojuwa India huwa ina mabingwa wa kutibu,lakini kama wanavyosema kwa ungonjwa huwo watoto wengi wakifanyiwa huwa hawaponi,,bora tusubiri Nusra ya Allah!Insha'Allah Mwenyezi Mungu akupe Tahfifu Sesilia!Jamani mimi nimestuka sana kuona Sesilia karudi bila kutibiwa imeniuma jamani,,najuta kwa nini nilikuwa nafuatilia hiki kitu,,,Tumuombeeni tu jamani,,,Mola Atamugh'afu!Hakuna kinachoshindikana kwake!Ahlam UK
ReplyDeleteKaka michuzi! katika maisha yangu sijawahi kumwaga machozi kila ninapomwona mtoto mpendwa cecilia mimi naomba kwa mungu mtoto cecilia apone juwa wewe umewagusa wengi sana na tunakuombea kwa mungu mimi niko mbali na TZ lakini ningekuwa na uwezo wa muhijiza ningefanya hili binti huyu apone, juwa tunakupenda na tuko na wewe kwenye sala zetu, mungu akinijalia nitakapo kuja TZ mwishoni wa mwaka huu nitakuja kukuona, nakuombea mtoto wetu cecilia,Amin
ReplyDeleteHoyce...Mungu akupe baraka zake. Cecy sasa ni kama mwanao. Nilijua wewe ni Binti makini ila kwa hili...take a bow! Hoyce ni mfano wa kuigwa na mama shupavu.
ReplyDeleteNimeumia mno moyoni kwa masahibu na maumivu ya binti yetu Cesy. Mungu aliyekutunza mpaka leo ataendelea kukutunza. Cesy uwe na amani.
Yaani kusema kweli inasikitisha sana na pia inatia huruma tunamuombea mungu azidi kumsaidia apone kusema kweli anateseka. Mungu ndiye muweza wa mambo yote hapa duniani atamsaida .
ReplyDeletemungu akupe nafuu ya haraka mtoto wetu cecilia,ila kama ni lishe ya muhogo ndo imekuwa chanzo cha ugonjwa wako basi watanzania wengi wenye kipato cha chini tupo katika shida ya kuugua magonjwa ya moyo.ila mungu atakujalia heri na dua zetu utapona mwanetu na hatuta choka kukuchangia ikiwezekana.watanzania tuzidi kumwomba mungu atusaidie especial sisi tunatumia muhogo kama breakfast na lunch wenye kipato duni.theresia
ReplyDeleteJamani kusema kweli anateseka lakini yote tumuachie mungu atamsaidia. Cecy mwamini mungu ni mkubwa atakusaidia mwanangu yeye ndiye tumaini pekee hapa duniani.
ReplyDelete