Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi,Bernedete Kinabo akiwa na Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi,Jafary Michael wakati wa kikao cha baraza la madiwani.
Watendaji wa halmashauri ya manispaa ya Moshi wakifuatilia kikao cha manispaa ya Moshi.
Diwani wa kata ya mji Mpya,Abuu Shayo akitoa hoja wakati wa kikao cha baraza la manispaa hiyo.
Wageni mbalimbali waliofika katika kikao hicho.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
Katika agizo la mkurugenzi,linataka wachafuzi wa mazingira kutozwa faini kati ya Sh 10,000 hadi 50,000 huku Meya akisisitiza kuwa azimio la baraza la madiwani limepitisha kuwa faini hiyo iwe kiasi cha Sh 10,000 kwa makosa yote ya uchafuzi wa mazingira.
Wakizungumza katika kikao cha baraza la madiwani la manispaa hiyo,mkurugenzi alisema faini hiyo imepitishwa kisheria na mabaraza yaliyopita na kwamba ili kutengua inatakiwa kubadilishwa kwa sheria hiyo.
Kauli hiyo ilipingwa na meya Michael kwa madai kuwa vikao vilivyopita vya baraza hilo vilipitisha azimio kwamba kiasi kinachotakiwa kutozwa ni Sh 10,000 na siyo vinginevyo kwani pia kazi hiyo haifanywi kwa uadilifu bali wachache kujipatia fedha.
Kutokana na hali hiyo,baraza la madiwani lilimtaka mwandishi wa kikao hicho kueleza jambo lililoandikwa kama azimio ambapo alieleza kuwa baraza limeazimia faini kuwa kati ya Sh 10,000 hadi 50,000 kauli iliyokataliwa na baraza na kutaka aandike Sh 10,000 pekee.
Wakichangia hoja hiyo Diwani wa kata ya Mji mpya, Abuu Shayo alisema pamoja na nia nzuri ya manispaa kutaka mji uwe safi lakini bado kuna baadhi ya wafanyabiashara na wananchi wamekuwa wakichafua mazingirabila adhabu yoyote.
“Siyo busara kwa wananchi kutozwa kiasi hicho cha fedha kwa kosa la kutema mate au kutupa uchafu mwingine wa aina yoyote wakati wanaosimamia zoezi hilo wanashindwa kuwadhibiti wanaotupa taka ngumuna kuziba mifereji ya maji ya mvua”alisema.
Hata hivyo kikao hicho kilisema kushuka kwa kiwango cha faini kwa wachafuzi wa mazingira hakuathiri faini kwa wanaoegesha magari bila taratibu(Wrong packing) na kutaka iendelee kuwa Sh 50,000 kama inavyoeleza sheria hiyo.
Katika hatua nyingine baraza hilo limesema linafanya mawasiliano na kampuni ya uwakala wa mazingira na uengeshaji wa magari ya Econ Consult ili kuwapa taratibu za kazi baada ya kubaini mapungufu kadhaa.
Meya wa mji ndiye bosi wa mji kwa maana anwajibika kwa wananchi moja kwa moja kwahiyo ana nguvu ya wananchi na mkurugenzi wa mji ni mtumishi tu wa serikali ameteuliwa na mtu mmoja serikalini kwahiyo hakutakiwa kuwa na sauti yeyote. inaelekea huyu mkurugenzi amekuwa akitumiwa na CCM kudhibiti nguvu ya chadema kuleta mabadiliko moshi mjini.
ReplyDelete