Mechi namba 78 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Simba iliyochezwa Oktoba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 337,537,000.
Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 53,366 ambapo kiingilio kilikuwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.
Baada ya kuondoa gharama za mchezo na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 51,488,694 na gharama za awali za mchezo sh. 27,405,250 kila timu ilipata sh. 77,592,916.
Mgawo mwingine ulikwenda kwa uwanja (sh. 25,864,305), TFF (sh. 25,864,305), Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF (sh. 12,932,152), gharama za mchezo (sh. 25,864,305), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam- DRFA (sh. 10,345,722) na Baraza la Michezo la Taifa- BMT (sh. 2,586,430).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. acha kampuni ichukue ligi tu, just imagine timu zimepata jumla ya 155,000,000/= ambayo ni chini ya 50% ya hela yote iliyopatikana(337,537,000). na ndo maana TFF hawataki kuachia hiki kitengo maana wao ndio mechi yao ya kupatia kipato.drfa wanapata mgao kwa lipi hasa???, huo mfuko wa maendeleo ya mpira wa miguu unafanya nn?sijawai kusikia chochote!!!! na pia huwa wanapata mgao kwenye mechi ya simba na yanga tu.
    dah kaka mithupu inauma sana!!!

    ReplyDelete
  2. Simba na Yanga Mnashindwa nini kujenga viwanja vyenu jamani?hata vya watazamaji 20000 tu.

    David

    ReplyDelete
  3. He kwa hakika bado unyonyaji upo nchini kwetu yanii kila klabu haikubata hata miliomni mia ambao ndio wavuja jasho?kwa hakika tutafika lakini baaado mbali sana.

    ReplyDelete
  4. IKIWA NI KWELI HIZO TIMU MBILI ZINAUWEZO WAKUPATA PESA KAMA HIZO KWANINI HAWA WACHEZAJI WA LION NA YOUNG AFRICANS WANAKULA KWA MAMA NITILIE NA KUTWA KUPANDA MADALADALA? MDAU TOKA BUJUMBURA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...