Waziri Mkuu mstaafu, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Cleopa Msuya (wa pili kulia), akihutubia katika mkutano mkuu wa mwaka wa 38 wa wanahisa wa kampuni hiyo, Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche na kutoka kushoto ni viongozi wa kampuni hiyo,na Katibu wa kampuni hiyo, Haruna Ntahena.
Mwanahisa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Eddy Mushi akichangia mada wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa 38 wa wanahisa wa kampuni hiyo, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Miradi Maalum, Phocus Lasway (kushoto), akifafanua jambo kuhusu mpango wa kuwasaidia wakulima wadogo wadogo wa kilimo cha shayiri nchini. zao hilo linatumika kutengenezea bia.
Mwanahisa wa TBL, Grace Nabur akichangia hoja katika mkutano huo.
Mwanahisa wa TBL, Mzee Kibonde kutoka Rungwe mkoani Mbeya, akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
Wafanyakazi wa TBL, waliofanikisha mkutano huo.
WADAU MNAONAJE HIYO PICHA YA TATU KUTOKA CHINI,NI USTAARABU KUSALIMIANA AU KUAGANA KUPITISHIANA MIKONO KAMA WALIVYOFANYA HAPO?
ReplyDelete