Dkt Harrison Mwakyembe akiwa na Mh Victor Mwambalaswa
Bungeni Dodoma siku zilizopita

Naibu  Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe leo amepelekwa nchini India kwa matibabu zaidi ya ugonjwa wa ajabu  uliomuanza  kiasi cha miezi mitatu iliyopita kabla ya hali kubadilika siku za karibuni na hatimaye mwili wake kunza  kuvimba na ngozi kuharibika.

Msemaji wa familia ambaye pia ni Mbunge wa Lupa Mh Victor Mwambalaswa amesema kwamba hali ya  ngozi Dk Mwakyembe ni mbaya, japokuwa ana nguvu zake na fahamu na anaongea bila shida na anatembea mwenyewe.

Viongozi kadhaa akiwemo Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli walikuwepo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar kumsindikiza Dk Mwakyembe, ambaye jana alitembelewa na Rais Jakaya Kikwete nyumbani kwake Mbezi Beach.

Kwa mujibu wa mke wa Dk Mwakyembe, Mama Linah Mwakyembe, daktari  wa mumewe amesema mgonjwa  anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi unaojulikana kitaalamu kama Exfoliative Dermatitis. 

 “Alianza kuugua muda mrefu kidogo, kama miezi mitatu iliyopita, hali hiyo ilikuwa inatokea na kupotea hadi sasa ambapo hali imekuwa mbaya zaidi,” alisema. 

Alisema madaktari waliomfanyia uchunguzi kwa nyakati tofauti katika kipindi hicho walitoa majibu tofauti na kuongeza kuwa wapo waliosema hali hiyo ilisababishwa na kisukari na mwingine ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kulikuwa na chembechembe za sumu katika damu yake. 

“Baada ya ngozi yake kubadilika sana na hali kuwa mbaya, tulienda hospitali na madaktari walitupa majibu tofauti, wapo waliosema ni kisukari na kuna mwingine alisema kuna chembechembe za sumu,” alisema Linah na kufafanua  kuwa daktari aliyedai hivyo hakuwapa maelezo zaidi. 

Kwa mujibu wa Linah, ngozi ya Dk Mwakyembe inawasha na inakuwa kama inatoa mba mwili mzima hadi kichwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Pole sana kiongozi wetu shupavu. Watanzania wenye uchungu na nchi yetu na rasilimali zilizomo tunakuombea kila la heri, upone haraka na urejee nyumbani kutusaidia kimaendeleo. Mungu akusaidie upone haraka mkuu. Tunakupenda sana.

    ReplyDelete
  2. pole dokta,kwanini india? Napatwa na mashaka na madaktari wetu,hayo ni majibu mawili tofauti kutoka kwa mabingwa wa afya zetu.huyo ni mtu mkubwa anapewa majibu kama hayo je mimi mzaramo toka chole itakuwaje.majibu yenyewe yanajionyesha kipimo kilikuwa ni macho,wa tz tumekwisha.

    ReplyDelete
  3. Pole mheshimiwa, hiyo ni kadar ya Mwenyezi Mungu

    ReplyDelete
  4. Pole sana mwanaharakati wetu wa ukweli,nakuombea kwa mungu inshallah utapona.Tupo pamoja Dr!!

    ReplyDelete
  5. Dr. Mwakyembe, nakushauri wewe na mkeo mwende Synagogue Church of All Nations (SCOAN), Lagos- Nigeria kwa Prophet TB Joshua UKAOMBEWE. Bwana YESU atakuponya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...