Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mama wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Professa Beno Ndulu kufuatia kifo cha mama yake mzazi Bibi.Regina Steven Mpangile kilichotokea juzi(30/9/2011) katika hospitali ya Hubert Kairuki jijini Dar es Salaam.Kushoto aliyesimama ni Professa  Beno Ndulu.Marehemu Regina anatarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya Kinondoni. Rais Kikwete alikwenda nyumbani kwa marehemu ,Tabata jijini Dar es Salaam kutoa pole na kuifariji familia ya marehemu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Gavana wa Benki Kuu Professa Beno Ndulu wakiwafariji ndugu na jamaa wa mama wa Gavana Marehemu Bibi.Regina Steven Mpangile nyumbani kwa marehemu Tabata jijini Dar es Salaam leo jioni.Maremu Bibi Regina alifariki juzi katika Hospitali ya Hubert Kairuki jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa kesho(jumatatu) katika makaburi ya Kinondoni. 
Picha na mdau  Freddy Maro wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...