Ndg. Mark K. Mfunguo mkazi wa Ubungo Msewe(karibu na kanisa la Deeper Life) amepotea tangu tarehe 01/10/2011 kabila lake ni mchagga wajihi wake ni maji ya kunde na ana mvi kichwani ana umri wa miaka 65 na ana tatizo la kupoteza kumbukumbu. Mara ya mwisho kuonekana ilikuwa ni tarehe 01/10/2011 siku ya jumamosi maeneo ya UBUNGO-EMAUS alipokwenda kwa ajili ya huduma ya maombi.
Mwenye taarifa zozote za kuonekana kwake atoe taarifa kwenye kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu naye na namba zifuatazo
0786-871720
0688-871720
0754484947
0713698240
0754-455176



Poleni sana wandugu. Huyo mzee inaelekea ana ugonjwa wa Alzheimer. Ni ugonjwa mbaya unaokuja kwa kasi sana. Kati ya watu mashuhuri waliowahi kuugua ugonjwa huu ni Rais Ronald Reagan wa USA, akafikia mahali hata hakukumbuka kama aliwahi kuwa Rais. Ugonjwa umeingia kwa nguvu sana Tanzania, mimi binafsi nina mgonjwa kama huyo, na nilikuwa nina mwingine aliugua hivyo hivyo kwa sasa ni marehemu. Naomba wanajamii na wanaharakati wauvalie njuga ugonjwa huo na kuhamasisha watu waufahamu kama kulivyokuwa na kampeni kuhusu magonjwa mengine. Sheria lazima zitungwe kuwalinda wagonjwa kama hawa. Ninauelewa kwa kuwa yamenifika nami ninauguza mpaka sasa. Mtu akimwona mgonjwa wako anaweza asijue kama ni mgonjwa anayehitaji msaada wa karibu wakati wote. Mara nyingi wanaweza kutapeliwa au hata kupata madhara kwa kuwa kumbukumbu zao zimepungua. Poleni sana na ninawaombea Mungu mfanikiwe kumpata mpendwa wenu.
ReplyDeleteUnasababishwa na nini? au unatokea tu?
ReplyDeleteI AM VERY HAPPY THAT MY UNCLE IS AT HOME AGAIN.
ReplyDeleteHE IS IN A FAIR CONDITION! HOME SAVE AND SOUND.
THANK YOU FOR THE FAST AND EFFICIENT RESPONSE.
JULIUS-SINA MUSHI (BERLIN-GERMANY)
kwahiyo mjomba amepatikana sasa hakuna maneno ndo unamaanisha mangi
ReplyDeleteHayo ni maradhi ya uzeeni ambayo yanawapata baadhi ya watu. Mtu anaweza kuchukua masaa kumi anazunguka hapo kwa hapo bila ya kujua anakokwenda au alokotoka. Fainali uzeeni!!
ReplyDeleteMy Uncle Mark is Safe and Sound at His home, Thanks to fast and efficient Action to the missing Person Report.
ReplyDeleteThanks God! We are all now calm and at ease.
Julius-Sina Mushi (Berlin-Germany)
Bado hawajagundua, ila chembe chembe za ubongo zinakufa taratibu siku hadi siku. Dawa zipo za kutuliza makali ila si kuponyesha kabisa.
ReplyDeleteWATU WENGINE BWANA! KWA KUOMBA WANANYENYEKEA LAKINI AKISHAFANIKIWA....ANAJIFANYA ANAJUA SAAANA.....KUOMBA KISWAHILI ILI KILA MTU AELEWE. LAKINI KUSHUKURU ALAS..POTELEA MBALI HATA WASIPOELEWA.
ReplyDeleteHii ndio huwafanya watu kudharau pale wanappomba msaada
Anonymous oct 03 07:00, wewe nawe hebu huko, huoni kama aliyeomba msaada na anayeshukuru ni watu wawili tofauti? Kwanza anayeshukuru anaishi Ujerumani alishasahau kiswahili mwenzio, hata report yenyewe kafanya kutafsiriwa..LOL
ReplyDeleteHUO UGONJWA WA Alzheimer UNAWAPATA WATU UZEENI KUANZIA UMRI WA 50 YEARS , MATUMIZI MAKUBWA YA POMBE/VILEVI NA VITU VYENYE CAFFENE SANA VINACHANGIA PIA.
ReplyDeleteUPO SANA MAREKANI BUT KWA SASA WATANZANIA WENGI SANA WANAUMWA NI KWA VILE TU HAKUNA VIPIMO VILIKWISHA FANYIKA.
MANGI-SINZA