Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti,Ephraim Mafuru (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 165 kwa Nahodha wa Timu ya Taifa,Mrisho Ngassa (pili kushoto) ikiwa ni sehemu ya Udhamini wa Kampuni hiyo kwa Timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo inajiandaa mchezo dhidi ya Morocco wa kuwania kufuzu kushiriki fainali za kombe la Mataifa ya Afrika zitakayofanyika kati ya Gabon na Equatorial Guinea mwakani.Wengine pichani ni Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa,Jan Paulsen (wa pili kulia) na kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF,Angetile Osiah.
Rais wa Shirikisho la Soka Nchini, Leodegar Tenga akizungumza na vyombo vya habari.
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa,Jan Paulsen akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na maandalizi aliyoyafanya kwa timu yake itakayomenyana na Timu ya Taifa ya Morocco hivi karibuni kuwania kufuzu kushiriki fainali za kombe la Mataifa ya Afrika zitakayofanyika kati ya Gabon na Equatorial Guinea mwakani.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti,Ephraim Mafuru akikabidhi vifaa vya michezo vitakavyotumiwa na Timu ya Taifa kwa Katibu Mkuu wa TFF,Angetile Osiah.
Nahodha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Mrisho Ngassa akielezea namna walivyojiandaa kwa mchezo uliopo mbele yao.

Na Francis Dande

Wadhamini wakuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kampuni ya Bia ya Serengeti leo imekabidhi mfano wa hundi yenye thamani y ash. Milioni 165 kwa ajili ya timu timu ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) inayojiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki fainali za kombe la Mataifa ya Afrika zitakayofanyika kati ya Gabon na Equatorial Guinea mwakani

Mbali ya kukabidhi hundi hiyo Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Ephraim Mafuru alikabidhi vifaa vya michezo zikiwemo jezi za mazoezi pamoja na viatu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya morocco utakaofanyika Okt. 9. Stars inatarajiwa kuondoka kesho Okt.6 kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika katika mji wa Marakechi nchini Morocco.

Nahodha wa timu hiyo, Mrisho Ngassa alisema kuwa timu imejiandaa vifuri na kuahidi kuwapa raha watanzania. Timu hiyo inakabiliwa na majeruhi watatu akiwemo beki wa kutegemewa, Shadrack Nsajigwa, Victor Costa, Juma Nyossa huku wachezaji Nizar Khalfan na Danny Mrwanda watakosa mchezo huo kutokana na kukosa ruhusu kutoka katika vilabu vyao, alisema Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Big up kwa Serengeti Breweries for the donations. Hizo football boots hazitafaa safari hii kwani mpaka mtumiaji azi-"break in" ili ziweze kutumika ipasavyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...