Penda usipende teknolojia imeleta mapinduzi makubwa sawasawa na wakati wa industrial revolution. Nchi nyingi zimepiga hatua kubwa kwa kuona umuhim wa kuwekeza kwenye sekta hii. 

Makampuni kama Amazon.com yamechukua full advantage of IT kutengeneza mamilion ya hela, kutoa huduma kwa jamii na kuajiri maelfu. Hata hivyo kusuasua na kusita kuwekeza kwenye teknolojia kumedhoofisha nchi nyingi na makampuni mengi.

Japokuwa hali ya uchumi wa dunia inayumba sana, watu wakiishi kwa hofu na mashaka, ni muhimu kuendelea kuhimiza uwekezaji kwenye sekta ya teknolojia. Viongozi katika sekta mbalimbali wamekuwa wakiona IT kama kitu ambacho ni kizuri kuwa nacho lakini sio muhimu sana. 

Kwa sababu hiyo imani imejengeka kwamba unawekeza zaidi kwenye IT pale unapokuwa kwenye hali nzuri kiuchumi na kuacha ama kutokuipa ICT umuhimu pale mambo ya kiuchumi yanapotetereka. ICT imekuwa victim kila inapotokea bajeti imeyumba.

Kwa kuendelea kuona kwamba IT au ICT sio chombo muhimu cha maendeleo, nchi na jamii zetu zimekuwa zikishindwa kuendana na kasi ya teknolojia. Hata tunapotaka sasa kuwekeza kwenye sekta hii wakati mambo yanapokuwa mazuri kidogo tunakuwa tumeachwa nyuma sana.

Kuwekeza kwenye ICT kunahusisha mambo makuu mawili:

1. Research in technology - hii ina-stimulate innovation

2. ICT/IT consumption - hii inahusisha education; infrastructures; hardware and software acquisation; n.k

Tunawahimiza viongozi kwenye private as well as public sector kubadilika na kujifunza kutoka kwa wengine. Inawezekana bajeti haitoshi, lakini kwa kui-sacrifice ICT ama kutokuona umuhimu wake ni vigumu ku-compete kwenye hii dunia ya leo.

Tunapenda kusisitiza kwamba ICT sio luxury bali chombo muhimu cha maendeleo. Tuendelee kuhimiza uwekezaji kwenye sekta ya teknolojia.

By Chief Editor at

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. umeongea jambo zuri sana,nilikuwa na hii idea ya kuandika article hasa kuilekeza kwa serikali na vyombo vya mawasaliano hasa kwa nchi zetu ambazo mambo kama haya ya teknolojia ya ICT wanaona kama ni starehe na hakuna jitihada yeyote inayofanywa kuboresha mifuno hii ya teknolojia,leo hii mtanzania anafurahia internet yenye speed 3Mbps na 1Gb ya kudownload kwa mwezi wakati wenzao speed ya kawaida ni 10Mbps na unlimited download,ni muhimu kufahamu katika ulimwengu tunaoelekea sasa technology kama hii itasaidia kuwafungua watu sana ili tuweze kushindana na dunia,asikudanganye mtu leo hii hata ukitaka kujifunza kutengeneza nuclear utapata elimu hiyo through internet na kwa sisi waafrika ambao maendeleo yetu yapo nyuma ni vizuri kuwekeza kwenye hii technology..wanafunzi wetu watapata kujua mambo mengi na sio tu hilo hata kubadilishana mawazo na wenzao nchi tofauti....inashangaza technology kama ya WIMAX ingetakiwa kuchnamkiwa sana maana ndio mkombozi kwa kuwa infrastructure zetu ni mbovu ila nashangaa watu wamelala tu wanabaki kusema tuna mkono sijui mkonga wa fibre optics!!!amkeni ndugu zangu kwenye 21 century internet inatakiwa iwe ndani hata kwa wale wanaoishi manzese kwa mfuga mbwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...