Tiketi kwa ajili ya mechi namba 78 kati ya Yanga na Simba itakayochezwa Oktoba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zitaanza kuuzwa kesho saa 4 asubuhi katika vituo vitano tofauti.


Vituo vitakavyouza tiketi hizo hadi saa 10 jioni ni Uwanja wa Taifa, kituo cha mafuta cha Oilcom Ubungo, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, kituo cha mafuta cha Big Bon kilichoko Msimbazi- Kariakoo na mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Samora/Ohio.


Pia tiketi zitauzwa siku ya mchezo katika magari maalumu yatakayoegeshwa katika maeneo ya uwanja. Tunatoa mwito kwa mashabiki kununua tiketi zao mapema ili kuepuka bughudha ya kuingia uwanjani siku ya mechi.


Viingilio katika pambano hilo ni sh. 5,000 kwa viti vya kijani na bluu (tiketi 36,000), sh. 7,000 viti vya rangi ya chungwa (tiketi 11,000) sh. 10,000 VIP C (tiketi 4,000), sh. 15,000 VIP B (tiketi 4,000) na sh. 20,000 VIP A (tiketi 700).


Waamuzi wa mechi hiyo ni Oden Mbaga (centre referee), Hamis Chang’walu (assistant 1) na John Kanyenye (assistant 2). Mtathimini wa waamuzi (referee assessor) ni Soud Abdi wakati kamishna wa mchezo huo ni Mohamed Nyange.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ngoma inaanza saa ngapi hii?Usiku au Saa 10 jioni?Mwenye jibu pliiz.

    David V

    ReplyDelete
  2. NI SAA KUMI JIONI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...