Meneja wa Vipindi wa Radio Clouds 88.4 Fm,Sebastian Maganga akionyesha kadi ya gari lake kwa waandishi wa habari,waliyokutwa nayo vibaka waliotaka kuiba gari lake lililokuwa limepaki kwenye eneo la kuegeshea magari,mchana huu.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Clouds Media wakiwa wamelizunguka gari la Polisi lililokuwa limewapakia vibaka hao ambao walishtukiwa haraka kutokana na gia waliyoingia nayo ya kujifanya wao ni mafundi wa gari hilo na wameagizwa na Sebasitian Maganga.
Askari Polisi waliofika eneo la tukio wakiwa na watuhumiwa hao ndani ya gari lao huku baadhi ya wafanyakazi wa Clouds wakiendelea kuwacheki vibaka hao bila hata ya kuwamaliza.
Vibaka wakiwa ndani ya gari la Polisi,cheki sura zao zilivyo,yaani hata hawafananii na kitu walichotaka kukifanya.
Gari ya Polisi likitoka ndani ya jengo la Clouds Media.
Gumzo likiendelea kwa wafanyakazi wa Clouds mara baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Msimamizi mkuu wa Madereva wa Clouds Media Group,Mzee Mrope akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio hilo ambalo alilishuhudia na kuamrisha askari wawaweke chini ya ulinzi vibaka hao mpaka Polisi walipofika na kuwachukua.
Seba inakuwaje unaacha kadi orijino ya gari ndani ya gari?acha kutuyeyusha.
ReplyDeleteNa wewe acha ushamba hiyo siyo kadi original.
ReplyDeleteHao msiwaite vibaka ni majambazi.
mbona hamjatuonyesha gari yenyewe?
ReplyDeleteBut they are very lucy boys....wameiba sehemu ya kistaarabu and surely its looks like they are treated in a very polite style.....lucky them!.....sipati picha ingekuwaje pale mujini Tandale!
ReplyDeleteMdau wa kwanza ile ni photocopy ya kadi na siyo orijino. Au kwa vile imekopiwa kwa rangi, si unaona muhuri kuonyesha kwamba ít is a true copy of the original?
ReplyDeleteLakini pia vijana wana moyo kweli kuingia kwenye mjengo na kutaka kujaribu bahati yao ya kuiba. Natamani hiyo akili yao wangeitumia kwa kitu kitachowaletea manufaa na siyo ujambazi.
Kweli kabisa hivi kwa nini Majambazi mnawaita vibaka???? Acheni kupoza lugha. Inabidi 'wahojiwe' hao ipatikane network nzima sio kuishia kwao tuu.
ReplyDeleteingekuwa vyema kama ungetuonyeshe gari ili sisi wenyewe tupime uzito wa hii kesi!?
ReplyDelete= = =
buffalo,
new york
Kwa hiyo na shughuli zote za clouds FM zilisimama. Yaani kama huku UK shughuli za SKY TV zisimame kwa kuwa mwandishi alitaka kuibiwa gari. Bongo Land
ReplyDeleteNami naungana na wachangiaji waliotangulia. Mngetuwekea na picha ya gari ili ilete mantiki. na wala msije mkatuambia kwamba hamkuiweka kwa sababu za kiusalama kwani kwa lugha hiyo nasi tutawauliza hizo za watuhumiwa mmeziweka na kuwaita vibaka kwa mantiki ipi na haki ipi.
ReplyDeleteWizi ni wizi regardless of the type of car
ReplyDelete