Meneja wa Azania Benki tawi la Masdo, Harun Mushi (mwenye miwani) akisakata rumba na mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa bonanza la wafanyakazi wa benki hiyo kwa matawi ya Dar es Salaam lililofanyika katika ufukwe wa hoteli ya Kijiji Beach iliyopo Kigamboni Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Wengine ni wafanyakazi wenzao wakiserebuka kwa mduara.
 Wafanyakazi wa matawi mbalimbali ya Benki ya Azania yaliyopo Dar es Salaam wakicheza mpira wa mikono majini wakati wa bonanza lilowakutanisha wafanyakzi hao lililofanyika katika ufukwe wa hoteli ya Kijiji Beach iliyopo Kigamboni Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


 Meneja wa Azania Benki tawi la Masdo, Harun Mushi wa timu ya mashabiki wa Manchester United akijiandaa kurusha mpira katika mpambano dhidi ya kombaini ya mashabiki wa timu nyingine Uingereza wakati wa bonanza la wafanyakazi wa benki hiyo kwa matawi ya Dar es Salaam lililofanyika katika ufukwe wa hoteli ya Kijiji Beach iliyopo Kigamboni Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Manchester walishinda kwa mabao 8 - 2.

Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Azania imefanya bonanza kwa wafanyakazi wake katika kuwapongeza na kuongeza ari ya kazi itakayoimarisha utendaji wa benki hiyo.

Wafanyakazi wa matawi mbalimbali yaliyopo Dar es Salaam juzi walijumuika pamoja katika ufukwe wa Kijiji Beach, Kigamboni Dar es Salaam ambapo pamoja na mingine michezo ya kuogelea,mpira wa miguu na kucheza dansi vilichukua nafasi kubwa ya bonanza hilo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Charles Singili ambaye hakuweza kufika katika bonanza hilo, Meneja wa tawi la Masdo Harun Mushi aliyemwakilisha alisema bonanza hilo ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano baina ya wafanyakazi.

Alisema mafanikio ya benki hiyo yanatokana na nguvu ya pamoja ya wafanyakazi katika matawi yao nchi nzima hivyo wakati fulani ni lazima nguvu hiyo ikutanishwe pamoja katika kufahamiana na kuimarisha umoja walionao.

Mushi alisema ni utaratibu ambao utakuwa unafanywa kwa vipindi kulingana na uwezo lakini uongozi utajitahidi kuwakutanisha wafanyakazi wake mara mbili hadi tatu kila mwaka kama uwezo utaruhusu kufanya hivyo.

"Ni bonanza la kufahamiana na kudumisha umoja na urafiki wa kikazi baina ya wafanyakazi, leo hapa wote ni wamoja bila kujali vyeo vyetu makazini, tunacheza, kunywa na kuogelea", alisema Mushi.

Kwa upande wake Magareth Izungu wa tawi la Masdo kitengo cha huduma kwa wateja alisema bonanza hilo ni sehemu nzuri ya kudumisha ushirikiano wa kikazi miongoni mwao.

Alisema kutokana na majukumu mengi ya kikazi wakati fulani unaweza usimfahamu mfanyakazi mnayefanya tawi moja hivyo bonanza hilo ni sehemu nzuri ya kuburudika na kudumisha mahusiano.

Katika baadhi ya michezo iliyochezwa, timu ya soka ya  wapenzi wa Manchester United iliichabanga bila huruma kombaini ya wapenzi wa timu nyingine Uingereza kwa mabao 8 - 2.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hongereni sana wana azania bank hii ni moja ya motisha kwa wafanyakazi tuongezeeni tu matawi mikoa yote napenda huduma zenu hasa kwenye mikopo

    ReplyDelete
  2. aaaaah mambo ya wana-azania si mchezo,yaani mmefurahi sana kwakweli na mmeenjoy,awaona kwa mbaaali vijana wa ifm enzi hizo,maganga na kimmosa,endelezeni kukutana namna hiyo hata mara 2 kwa mwaka ili upendo udumu ofisini

    ReplyDelete
  3. Kuna anayejua kuogelea hapo??

    ReplyDelete
  4. Wana azania msisubiri family day ndio mle tizi hebu angalieni miili yenu ilivyo bumpy punguzeni minyama hiyo nyie bado vijana sana kuwa na minyama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...