Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Prof Jumanne Maghembe (wa pili kulia) kwa pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Ephrahim Mafuru (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni hiyo Teddy Mapunda (kulia) wakigonganisha chupa za kinywaji cha Pilsner Lager baada ya kukizindua katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Meneja wa Pilsner Lager Maurice Njowoka.


Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kinywaji cha Pilsner Lager na kuahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali zinazogusa mambo mbalimbali ya maendeleo katika kupunguza ama kuondoa kabisa umasikini uliokithiri miongoni mwa jamii ya kitanzania.

Kinywaji cha Pilsner Lager pamoja na vingine vinavyozalishwa na kampuni hiyo vitaongoza mapambano ya kupunguza umasikini wa watanzania kwa kurudisha faida wanayopata katika mambo tofauti ya kimaendeleo.

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Ephrahim Mafura aliyasema hayo wakati wa uzinduzi maalumu wa kinywaji cha Pilsner Lager katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mafuru alisema kuzinduliwa kwa kinywaji hicho kinachotumia slogan ya ‘kinywaji imara kama simba’ ni matumaini mapya kwa watanzania kwani wamedhamiria kuyafanya maisha ya watanzania kuwa imara kama Simba.

“Kampuni ya Serengeti ni miongoni mwa wadau wakubwa wa maendeleo nchini ambao tumedhamiria kuendelea kuongeza nguvu ya uzalishaji itakayotufanya tupate faida zaidi na kusaidia zaidi watanzania,”

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Prof Jumanne Maghembe aliishukuru kampuni hiyo kwa mchango wake katika maendeleo ya nchi na kuwataka wadau wengine kuunga mkono jitihada hizo.

Alisema serikali inatambua na kuthamini mchango wa maendeleo wa kampuni ya Serengeti kwa watanzania na kwamba wakati wote serikali inaunga mkono wadau wa aina hiyo na wizara ipo wazi na huru kupokea maoni ya kuboresha huduma za kimaendeleo.

“Mmekuwa wadau wakubwa wa maendeleo nchini, mchango wenu unatambulika na kuthaminiwa na serikali kwani changamoto tulizonazo zinahitaji nguvu ya pamoja, hongereni kwa kujitolea na tunatoa wito kwa wengine kufuata nyayo zenu,” alisema Waziri Maghembe.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni hiyo Teddy Mapunda  alitaja baadhi ya michango ya maendeleo ya kampuni hiyo kwa watanzania kuwa ni pamoja na kurahisha soko la malighafi ya wakulima wa ndani ambao sasa wanauza shayiri na mtama kwa kampuni hiyo.

Pamoja na hayo alisema SBL imekuwa ikifadhili masomo ya elimu ya juu lakini pia imekuwa na mchango mkubwa katika kuzalisha nafasi za ajira kwa watanzania waliopo maeneo ya Dar es Salaam, Moshi na Mwanza vilipo viwanda vyao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...