Wafanyakazi wa TICTS tokea jana wamekuwa na mgomo wa kufanya kazi katika Kitengo hicho Bandari wakishinikiza kulipwa madai yao ya Hisa ya zaidi ya miaka Miwili.

Taarifa kutoka kwa wafanyakazi hao zinasema kuwa, licha ya kugoma kwao lakini uongozi wa Kitengo hicho bado haujawaita ili kupata suluhu ya tatizo hilo na badala yake umekutana na Uongozi wa wafanyakazi (Dowuta) TICTS pekee.

Wafanyakazi hao wanaodai kuwa wataendelea na Mgomo huo mpaka hapo watakapolipwa Stahili zao na Kitengo hicho. 

Kufuatia mgomo huo shughuli zote za Kitengo hicho cha TICTS zimesimama Pia katika mgomo wao Hawataki baadhi ya viongozi wao kwa sababu ya unyanyasaji, wameomba serikali iingilie kati na ikiwezekana wawaondoe viongozi hao ambao Ni Biset Nevil, Anton,Mzungu wa Security,mama Prediganda Asenga na Abel Mwangwa maana hao ndo wachochezi wakubwa ili hisa zao wasipewe wagawane na mafisadi wa nchi hii na pia wanaomba serikali iingilie kati maana wazungu wao wanalipwa mishahara mikubwa na wakati kazi hufanya wao,utakuta mzungu mmoja analipwa dola za marekani elfu ishirini na sita $26,000 kwa mwezi huku wafanayakazi wakitaabika na kufukuzwa ovyo kama kuku.

"Bado mgomo uko pale pale mpaka kieleweke maana walikuwa wanasingizia serikali na wenye share ambao ni akina Karamagi na wengine sasa kama hao ndo chanzo basi waende wakaongee nao na watae sababu ya kuzuia hizo asilimia tano tulizosign nao mkataba kwamba wakifika miaka kumi watatupatia wafanyakazi asilimia tano"alisema mmoja wa wafanyakazi hao. Hizo ailimia tano zinathamani ya sh. billion 16.7
Mgomo ukiendelea.
Sehemu ya Mabango yanayotumiwa na wafanyakazi hao wakati wa mgomo huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. MMEMSAHAU MAMA SHITINDI!!MICHUZI ONGEZEA HILO JINA KWENYE LIST YAKO.

    ReplyDelete
  2. Kumekucha TICTS, Big up wafanyakazi hawa mafisadi sisi tumewachoka nchini? Wananyanyasa wafanyakazi, mishahara midogo wao wanaondoka na minono

    ReplyDelete
  3. Ehee makubwa!!!! Hapa serikali ielewe kuwa watu sasa wameamka hamna anayetaka kuonewa sasa

    ReplyDelete
  4. MPAKA KIELEWEKE! SIO NINYI TU HATA WAFANYA KAZI WA MAHOTELI MAKUBWAMAKUBWA KAMA SEACLIFF,COLDEN TULIP,MOVENPEAK, WAFANYA KAZI WAONEWA SANA VIONGOZI WAO MISHAHARA MINENE NAO NI PESA YA DALADALA TU NAULI-UNIFORM ZA BURE BASI

    ReplyDelete
  5. Aghhhhh, tanzania uozo mtupu. Kuweni na msimamoooo. Mi ndo maana sitaki kurudi bongo bora niendelee kubeba box, unyanyasaji mtupu. Hawa wawekezaji watakula mpaka lini?

    ReplyDelete
  6. Weraaa hii ni story au kweli??? Kama kweli binafsi nawapongeza sana hao wafanyakazi ka jitihada nzuri. Tumechoka kuonewa na kunyanyaswaaaaa

    ReplyDelete
  7. jamani Tanzania tumefikia wapi sasa hadi kazi ya security inaongozwa na mzungu hii ni aibu kubwa kwa taifa kushindwa kulinda ajira za raia wake.

    ReplyDelete
  8. Tudai madai mazuri ila tuache uvivu,wizi na ubabahishaji uliobobea jamani.

    ReplyDelete
  9. We Anonymous Wed Oct 26, 12:37:00 PM 2011, Huko ulaya utaliwa mpaka lini wenzako wajanja wanakuja bongo wanatengeneza bingo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...