Wahariri wa vyombo vya habari nchini,wakitembelea kiwanda cha bia cha TBL,wakati wa ziara yao. `
 Mtaalamu wa Mafunzo ya Utengenezaji bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Rose Mrina (wa pili kulia), akimuelezea Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya magazeti ya New Habari, Deodatus Balile jinsi kiwanda cha bia kinavyofanyakazi, wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari Makao Makuu ya TBL, Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la The Guardian, Wales Maugo na Mnaku Mbani ambaye ni Mhariri wa gazeti la Business Times.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche (kulia), akibadilishana mawazo na Mhariri gazeti la The East African, Joseph Mwamunyange (katikati), pamoja na Mhariri Mtendaji wa kampuni ya New Habari, Deodatus Balile baada ya kufanya mkutano na wahariri wa vyombo vya habari, katika Makao Makuu ya TBL, Dar es Salaam, ambapo aliwaeleza kuhusu utendaji na mafanikio ya kampuni hiyo.
 Mtaalamu wa Mafunzo ya Utengenezaji bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Rose Mrina, akiwaelezea wahariri kuhusu zao la shayiri linalotumika kutengenezea bia. 
 Wahariri wakiwa chumba cha kompyuta zinazotumika kupikia bia katika kiwanda cha TBL
Meneja Miradi Maalum wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo (kulia), akielezea mbele ya wahariri wa vyombo vya habari,kuhusu jinsi TBL ilivyoweka kipaumbele chao kusaidia jamii katika miradi ya maji nchini. Wahariri walialikwa kutembelea kiwanda cha bia kilichopo Makao Makuu ya TBL, Dar es Salaam 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...