Miili ya watu 12 walioteketea kwa moto katika ajali ya basi la Deluxe Coach iliyotokea Misugusugu mkoani Pwani juzi, watazikwa leo na Serikali kwa heshima zote katika kaburi moja katika eneo la Air Msae mjini Kibaha.
Eneo hilo ndipo walipozikwa watu waliopata ajali ya basi la Air Msae lililokuwa likitokea Arusha kuja Dar es Salaam miaka ya 1990.
Uamuzi huo umefikiwa na kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Pwani, iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mh. Mwantumu Mahiza kutokana na miili hiyo kuharibika vibaya na kushindwa kutambulika.
Mh. Mahiza alisema kabla ya maziko, miili ya watu hao itachukuliwa sampuli kwa ajili ya vipimo vya vinasaba (DNA) ili vifanikishe utambuzi wao.

Wananchi na polisi wakiangalia mabaki ya basi hilo baada ya kuteketea kabisa kwa moto.

Mmoja wa watu waliokuwa wakitoa mabaki ya miili ya watu walioteketea kwa moto akiendelea na zoezi la kuangalia iwapo kama kuna masalia yeyote.
Basi liliteketea kabisa na mabaki ya miili ya watu ililazimu kukusanywa kwa beleshi.
Picha zote na Yassin Nicas Mtei
jamani jamani ajali za kizembe zinapoteza maisha ya watu wasio na hatia,huu ni uzembe baina ya dereva na abilia kwasababu kama gari lilikuwa mwendo kasi kwanni abiria wasingepiga simu polisi? au wamsimamishe dereva...yaonekana abiria walifurahia huo mwendo kwani sijasikia mjeruhi akisema walimkataza dereva kwenda mwendo kasi...
ReplyDeletejamani jamani ajali zinatumaliza, huu ni uzembe kati ya abiria na dereva kwani sijasikia mjeruhi akilalamika kuwa walimkataza dereva kuendesha mwendo kasi inaonesha walifurahia
ReplyDeleteJamani ni ajali mbaya na natoa pole kwa wafiwa wote, serikali ya tanzania na mwenye mali. Hili naomba Kamanda wa Plisi wa Mkoa wa Tanga liwe angalizo kwake kwani analala mno usingizi, Vibasi maarufu vya Noah Tanga kwenda Korogwe vinajaza mno hadi vigoda vinawekwa pale kwa dereva kiasi hata likitokea la kutokea dereva anashindwa kumanuva kwani anakua kakaa upande kabisa na trafikiwapo wanaona.
ReplyDeleteMarehemu hao japo kisura imekuwa ngumu kuwatambua,je majina yao hayakutambuliwa pia?Maana sheria inasema abiria wote waandikwe majina wakati wa kukata ticket.Tunaomba kujua majina ya watu waliokufa kama yalivyotolewa kwenye orodha ya wasafiri waliokata ticketi
ReplyDeletemwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahala pema peponi,AMEN!!
ReplyDelete