Hapa ni Kinondoni Manyanya karibu kabisa na mataa ya kuongoza magari ambako kila siku ukipita ni lazima ukutane na mambo haya,na sijui ni sababu ipi inayowapelekea wawekaji wa taka hizi waone kama hapa ndio sehemu sahihi ya kutupia uchafu wao huo.Hali hii ipo katika maeneo mengi ya jiji la Dar na inazidi kuenezwa siku hadi siku.sasa kwa mpango huu jiji hili litafanikiwa kuwa safi??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mdau Mwenzangu hii, inaonyesha kwamba, wananchi wapo mbele zaidi katika kufikiri kuliko serikali za mitaa hiyo, hawa watu kwa matendo wana ishauri serikali ya jiji kuwa na magari ambayo yanazunguka kubeba takataka hizo, ndivyo wanavyo fanya wenzetu huku majuu na ni kitu kizuri kimaendeleo, hapo siyo kwamba wanatupa hapana wanaweka zipatekuchukuliwa kupelekwa huko dampo. upo hapo, I like that.

    ReplyDelete
  2. Wananchi hawa hawana pa kupeleka taka zao, njia mbadala ndio hiyo. Nawapa hongera sana kuliko kutupa taka ovyo tu. Ona walivozifunga vizuri. Serikali ya amtaa bongolala.

    ReplyDelete
  3. me too i like that mdau wa kwanza umesema kweli sasa kazi waifanye serikali kupitisha sheria ya uzoleshaji wa taka. i like that heko wawekezaji wa taaka hapo

    ReplyDelete
  4. Zamani tulikuwa na magari ya kuzoa taka na mapipa ya taka tulikuwa tunapata kwa ajili ya kuwekea taka sasa leo tunakaribia miaka 50 toka tupate uhuru hayo ndio mafanikio yanayoonekana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...