Sanamu ya kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Msumbiji Hayati Samora Machel jijini Maputo baada ya uzinduzi wake Oktoba 19, 2011 ambapo wasanii Carolla kinasha na Paul Ndunguru walishuhudia na kushiriki katika tamasha la Umoja Music Festival lililoenda sambamba na uzinduzi huo
 Msanii Paul Ndunguru (kulia) akiwa na gwiji la muziki toka Zimbabwe Oliver Mutukudzi kwenye tamasha hilo
Paul Ndunguru (wa tatu shoto) na Carolla Kinasha wakijumuika na wanamuziki Ray Phili (shoto) na Oliver Mutukudzi jukwaani (wa tano toka shoto) pamoja na wasanii wengine kwenye tamasha hilo.

Wasanii maarufu wa muziki halisia,  Paul Ndunguru na Da' Karola Kinasha hivi karibuni wamemetoka Maputo, Msumbiji, kwenye tamasha kubwa la muziki la Umoja Music Festival linalofanyika kila mwaka likijumuisha nchi ya Kenya Uganda,Afrika kusini na wenyeji Msumbiji.

Wasanii hawa wanajisikia kupata heshima kubwa kuimba na magwiji kama Oliver Mutukuzi wa Zimbabwe na Ray Phiri wa Afrika kusini ambaye ni mpiga gita na mwimbaji,  ambaye ndiye  aliyetunga na kutengeneza nyimbo sita kwenye album ya 'Grace land'  iliyompa umaarufu,  heshima na utajiri nguli wa muziki Paul Simon, wakati huo akiwa katika harakati za  kushinikiza Nelson Mandela aachiwe huru. 

Ray Phiri anasema "najivunia kwa jinsi (Mandela)  alivyotoka jela, niliuza haki miliki ya nyimbo kwa mzungu huyo. Hivyo hivyo nilimtumia mzungu kupata nichotaka kwa nchi yangu, Mandela anatambua hilo" mwisho wa kunukuu.

Lingine kubwa waliloshuhudia Paul na Carolla ni uzinduzi wa sanamu ya kumbukumbu ya Rais wa kwanza wa Msumbiji, Hayati Samora Machel, iliyo zinduliwa tarehe Oktoba 19, 2011. Katika sanamu hiyo Hayati Samora anaonekana akiwa amenyoosha kidole kimoja kukumbuka maneno yake aliyosema."Kama ninapata kilo moja ya mchele, basi kila Mmozambiki apate kilo moja ya mchele"

Paula na Carolla wanasema inaleta raha kuona jinsi wananchi wa Msumbiji wanavyomuenzi shujaa wao na wanajiuliza sisi watanzania tunamuenzi vipi BABA WA TAIFA? Hawapendi i kuzungumzia kwama sanamu hii,   kama ile ya Dr Martin Luther king jr kule  Washington kuwa imetengenezwa na Mchina, licha ya kwamba Wamakonde wa 'Nchumbiji' kuchonga masanamu ndio kazi yao......

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...