Mshindi wa Tatu wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula, Bi Anna Oloshiro kutoka kijijiji cha Parakuyo, wilayani Kilosa akipokea Solar Panel kutoka kwa Afisa Kampeni na Utetezi wa Shirika la Oxfam (Tanzania), Lilian R. Kallaghe.
Mshindi wa Kwanza wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula, Esther Jarome Mtegule akifurahia na mumewe Beatus Masima mara baada ya kukabidhiwa Power Tiller na Shirika la Oxfam. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Bibi Dari Rwegasira na Mkurugenzi wa Shirika la Faraja lililosambaza fomu za shindano hilo kwenye vijiji vya wilayani Mpwapwa. Shindano hilo la aina yake liliendeshwa na Oxfam na washirika wake hapa nchini kwa lengo la kutambua mchango wa wanawake wakulima na wafugaji wanaochangia uhakika wa chakula nchini. Jumla ya wanawake takriban 7,000 kutoka Tanzania Bara na Visiwani walishiriki. Mshindi wa kwanza alipata Power tiller na washindi wa Pili na wa Tatu kila mmoja alipata Solar Panel.
Zawadi siku hizi zimekuwa nyingi!!
ReplyDelete