Watanzania wanaoishi Australia wameipongeza Serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kukuza kwa kiasi kikubwa uhuru wa habari ambao unawawezesha kupata habari za uhakika kutoka nyumbani wakati wote wanapozihitaji.
Watanzania hao pia wamempongeza Rais Kikwete kwa maendeleo makubwa ya nchi wakati wa uongozi wake na hasa maendeleo ya uchumi ambayo yameiweka Tanzania miongoni mwa nchi 10 duniani ambazo chumi zake zinakua kwa kasi zaidi duniani.
Pongezi hizo kwa Rais Kikwete na Serikali yake zimetolewa leo, Jumatano, Oktoba 26, 2011 na Watanzania wanaoishi katika Jimbo la Australia Magharibi wakati Rais Kikwete alipokutana na kuzungumza nao kwenye Ukumbi wa University Club wa Chuo Kikuu cha Western Australia, eneo la Crawley, mjini Perth.
Katika risala yao iliyosomwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Bw. Asimwe KAbuga kwa Rais Kikwete, Watanzania hao wamesema: “Mheshimiwa Rais, tunakushukuru sana kwa msimamo wako wa kulea na kuendeleza uhuru wa habari na wa vyombo vya habari nchini na uvumilivu wako wa uhuru huo.”
Akizungumza na Watanzania hao, Rais Kikwete amewataka Watanzania hao wa Australia na wengine wote wanaoishi nje ya nchi kujua kuwa wajibu wa kuiendeleza Tanzania ni wajibu wa Watanzania wote wanaoishi ndani na nje ya nchi.
Amesema kuwa wakati mwingine baadhi ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi wamekuwa wanajifanya kama vile hawana wajibu wa kuiendeleza Tanzania na kuwa yuko mtu maalum wa kuifanya kazi hiyo ya kuiendeleza nchi.
“Mnajifanya wakati mwingine kuwa nyie hamna wajibu wa kuiendeleza nchi yetu. Nimepata kuwauliza wenzenu sehemu nyingine kuwa huyo mtu ambaye mlimwachia nchi yenu ili aiendeleze ni nani ili iwe nzuri zaidi ndipo muweze kurudi?
Rais Kikwete amewakumbusha Watanzania hao kuwa kaulimbiu yao inatakiwa kuwa: “Ishi Ughaibuni, Lakini Msisahau Kwenu,”na akawakumbusha baadhi ya mambo ambayo Mheshimiwa Rais amesema ni muhimu kwa Watanzania wanaoishi nje kuyakumbuka.
Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na kuwataka Watanzania hao kutokusahau nyumbani kwao kwa maana ya kupatengeneza kwao ili kama wanataka kurejea nyumbani wawe na mahali pazuri pa kufikia.
Hata hivyo, Rais Kikwete amekiri kuwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanakabiliwa na changamoto kadhaa katika jitihada zao za kujenga nyumbani ikiwa ni pamoja na ukosefu wa viwanja na wakati mwingine kutokuwa na watu waaminifu wa kusimamia miradi yao ukiwamo ujenzi wa nyumba.
Rais Kikwete amewataka Watanzania hao kuchangia uchumi wa nchi yao kwa kupeleka akiba ya fedha nyumbani, kuwekeza ama kutafuta wawekezaji, kuchangia uchumi kwa kutumia ujuzi wao ambao wameupata katika muda wao wa kuishi nje na pia kupeleka nyumbani teknolojia mpya zinazoweza kusaidia nchi.
Kuhusu suala la uraia pacha (dual citizenship), Rais amesema kuwa suala la uraia ni suala la Kikatiba na hivyo litaamuliwa tu katika Katiba mpya ambayo mchakato wake wa kuijadili utaanza karibuni. “Hili siyo suala la Rais, bali ni suala la Kikatiba. Uraia ni jambo kubwa kuamuliwa na Rais, na wala haliko katika mamlaka ya Rais hata kama ni jambo la manufaa kwa sababu ni jambo halina hasara kwa yoyote.”
Hata hivyo, Rais Kikwete ameonya kuwa suala hilo siyo rahisi sana kwa sababu halipokelewi vizuri na baadhi ya wananchi nyumbani ambao wanaona kuwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanataka kunufaika pote pote. “Mawazo kuhusu suala hilo yamewagawanyika sana miongoni mwa wananchi.
Kuhusu suala la Watanzania wanaoishi nje kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali imepokea ombi hilo na litashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu na kanuni zilizopo.
Rais Kikwete pia amewaomba Watanzania waishio nje ya nchi kuwa watu wema na wenye kuzingatia sheria, kanuni na taratibu. “Hatuko tayari kutetea waharifu na watu wanaovunja sheria katika nchi za watu wengine kwa sababu hata kule nyumbani hatuwatetea waharifu. Ukiiba, utafungwa. Ukibaka, utafungwa. Ukiuza madawa ya kulevya, utafungwa na katika nchi nyingine watu wanaopatikana na hatia hii hunyongwa.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Ukionewa, tutakutetea. Lakini, ukifanya uharifu hatutahangaika na wewe kwa sababu hata kwetu watu wanaobaka tunawafunga maisha, wanaouza madawa ya kulevya, tunawapa vifungo vya muda mrefu. Kuweni raia wema, ishini kwa mujibu wa sheria.”
Rais Kikwete yuko nchini Australia kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Madola – CHOGM, ambao unaanza keshokutwa mjini Perth.
Mmesikia alichowambia Rais wetu lakini?..najua atakuwa amewagusa.Ni ukweli..Rafiki zangu wa Australia wengi mnashindwa kweli kurudi nyumbani sijui kwa nini..;Rafiki yangu mmoja yuko huko nilimwuliza swali akaniambia eti nauli ni kubwa kusafiri kurudi nyumbani-TRUE or FALSE?.
ReplyDeleteDavid V.
warudi nyumbani , kuna opportunities gani nyumbani? umeme tabu , maji tabu , matibabu tabu , kazi azipatikani na ukipata malipo madogo , sasa wewe unaosema watu warudi nyumbani umewataarishia nini uko nyumbani cha kuwafanya warudi
ReplyDeletemdau uswiss
Viongozi wetu wengi wanakuja kutuasa kwamba tujenge nyumbani sisi wengi tuko na majumba sio nyumba lakini na wao hawatujali sbb lazima wajue kwamba haturuhusiwi hata kufungua A/c tanzania sasa tumeinvest nchi yetu lakini pia nihasara kwetu sbb hatuwezi hata kupata mikopo ama kufungua A/c na hili swala wanalijua sio kwamba hawalijui sasa nikama wanatukejeli tu kila siku!Tangu enzi za mkapa alikuwa akija anatwambia hivyo lakini hawatujali sbb hawatushughulikii bora mchina anashughulikiwa kuliko sisi!kwakweli viongozi wetu naona yanawatoka maneno bila Nolegi inasikitisha sana!
ReplyDeleteNikweli Australia ni mbali na nauli ni ghali mno.Pia acheni mawazo ya mwaka47 kwamba kila alie nje anachonyota kuku kwa mrija.Mimi nimkenya wa Mombasa na mzazi wangu1 ni Mtz nafanya kazi hapa profession na ninaurai hapa lakini maisha sio rahisi kihivyo sembuse mpiga box.So msiwalaumu wenzenu tu watu wengine wanapata hela yakusogezea siku tu na wengine hufanya kazi za taxi.
ReplyDeleteI cannot believe the gentleman on the left hand side fell asleep while the President was speaking, hiyo siyo heshima hat kidogo. Yes Asustralia is very very far it costs a lot to travel back Bongo, but that is not an excusee of not going home at least once every 2 or 3 years.
ReplyDeletebetter kujanga au kununua abraod than TZ. its chaeper abroad lol
ReplyDeleteWakubali tu uraia wa nchi mbili mbona tutajenga!! kwa hali ya sasa ukiwa raia huku hata hicho kiwanja tz huwezi kununua.
ReplyDeleteTunajengaje wakati kila kitu hewa Tz? ukinunua kiwanja hewa,ukiomba ndugu akununulie anatumia hela zetu vibaya. Viwanja vipo ila hatuvipati wanapata wachina.eeeehe heeeehe
ReplyDeleteUnashangaa mtu kulala wakati Raisi anazungumza? Hapa nyumbani wabunge wanalala bungeni wakati wananchi (waajiri)wao kibao tunawaangalia tukitegemea wasimamie maslahi yetu. Labda ni kautamaduni ketu, kutokuzingatia sehemu za kulala...
ReplyDelete