Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) , Marcio Maximo kwenye hoteli ya JW MARRIOTT ya Rio de Janeiro akiwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil Leo.Katikati ni mkewe Mama Tunu Pinda.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars), Marcio Maximo kwenye hoteli ya JW MARRIOTT ya Rio de Janeiro akiwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil Oktoba 8,2011.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
AH MAXIMO MBONA TUNAKUKUMBUKA MAANA ULIVYOONDOKA NA SOKA LA BONGO LIKAONDOKA INGELIKUWA AMRI YANGU NINGELIKURUDISHA UTUFUNDISHIE TAIFA YETU KWA MIAKA 10 NAZANI HATA KOMBE LA DUNIA TUNGEFIKA TUNAOMBA MZEE PINDA MJULISHE SOKA LETU LIMEDODA TOKA ATOKE YEYE NI SAWA KAMA TULIRUKA MAJI TUKAKANYAGA MATOPE mdau Richie wa ughaibuni
ReplyDeleteBring him back!!!!!
ReplyDeleteWadau wanaosema Maximo aliendeleza soka la TZ sikubaliani nao kabisa. Maximo ndio aliliharibu soka letu kwa visingizio vya nidhamu na kuita wachezaji wachanga. Hakuwa na timu kamili yaani first eleven inayotambulika kama ilivyo kwa sasa kwa kocha Poulsen, mimi namwona Poulsen ni zaidi ya Maximo.
ReplyDeleteNapenda Mama Pinda alivyovaa T-Shirt yenye bendera ya Tanzania. Hongera Mama!
ReplyDeleteMdau wa sun oct 9,01:37PM... Sasa kama wachezaji wetu hawana nidhamu mnataka msiambiwe. Huu udekezaji wa wachezaji sababu wana majina ndo unasababisha udumaaji wa soka la Tanzania. Mchezaji mlevi hana adabu kwa viongozi na haheshimu kanuni za mpira unataka aendelewe kupangwa. kuna mifano ya wachezaji waliopigwa chini na mataifa na vilabu vingi duniani kwa sababu za kutokuwa na nidhamu wala heshima.
ReplyDelete1. Romario alipigwa chini na kocha Big Phil Scolari sababu ya kutokuwa na nidhamu.
2. Nicklas Bendtner, Adebayor, Jermaine Pennant, David Bentley hawa wote walisota benchi na mwishowe kuuzwa na Arsenal sababu mojawapo ni kutokuwa na nidhamu.
3. Adriano alipigwa chini na kocha wa Brasil (World cup 2010) kwa kutokuwa na nidhamu.
4. Mfano mwingine ulio hai sasa hivi ni TEVEZ. Pamoja na kuwa na kipaji, nidhamu yake ni ndogo sana.Hakuna kocha anayetaka ile mbegu katika timu yake.
*** Sasa vichezaji vyetu ambavyo havijulikani nje ya Tanzania vikileta maroroso katika timu bado mnataka vipewe nafasi sababu vinachezea Simba au Yanga.
Kama mambo yenyewe ndo haya tutabaki kuangalia wachezaji wa wenzetu katika luninga.
Hapa Tz kwa soka hili inabidi Benitez aje..au unasemaje Michuzi wa Anifield.
ReplyDeletemi nawaona wote choka bora julio kiwelu msema ovyo
ReplyDeleteAh nakubaliana na mdau wa hapo juu, wachezaji hawana nidhamu hata kidogo (ulevi, bangi, jeuri) lakini bado munataka watetemekewe.
ReplyDeleteMaximo ndiyo wa kwanza angalau kuweka hiyo nidhamu. Hivi sasa kidogo ndiyo vimeanza kuingia akilini. Lakini mwanzilishi siku zote haonekani kufanya kitu.
Ila naona amenenepa kidogo.