Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Mh Tim Clarke akiweka shada la maua mwenye kaburi la Baba wa Taifa kijijini Mwitingo, Butiama, leo kwa niaba ya mabalozi wote wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania. Picha na Mindi Kasiga
Leo dunia imetoa heshima kwenye kaburi la Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere nyumbani kwake  Butiama Mkoani Mara, ambapo Jumuiya ya Kimataifa Tanzania inafanya ziara ya siku tatu mikoa ya Mara, Manyara, Arusha na Zanzibar kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru.
Ujumbe huo wa mabalozi zaidi ya thelathini wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe (Mb,) waliweka mashada ya maua kwenye kaburi la Hayati Mwalimu Nyerere pamoja na kutembelea jumba la makumbusho kumuenzi Baba wa Taifa.
Kwenye hotuba yake kwa wageni, Mhe. Membe alisema “Watanzania kamwe hatuwezi kusherehekea miaka 50 ya uhuru bila kutambua mchango wa Mwalimu Nyerere. Na kwa kuileta dunia Butiama leo, kwa kweli tumemtambua na kumuenzi Baba wa Taifa.”
Wakiwa kijijini  alipozikwa Baba wa Taifa, mabalozi hao pia walitoa salamu zao kwa familia na kwa Mama Maria Nyerere, wakielezea mchango wa Mwalimu Nyerere kwenye nchi zao, ambapo Balozi wa India nchini alitoa zawadi kwa Mama Maria Nyerere .
Naye Balozi wa Palestina Tanzania Mhe.Dk. Nasri Abujaish amesema kutokana na mchango mkubwa wa Baba wa Taifa aliotoa nchini kwake Palestina, na urafiki uliokuwepo baina ya Hayati Mwalimu Nyerere na Muasisi wa Taifa la Pakestina Hayati Yasin Arafat, nchi yake imeamua kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuupa jina la Nyerere mojawapo ya barabara kuu za Mjini Ramallah, Palestina.
Naye Mama Maria Nyerere akiongea na vyombo vya habari alisema amefarijika sana na ujumbe huu mkubwa kufika kijijini kwake, na kutambua mchango wa Baba wa Taifa, miaka 12 baada ya kifo chake.
Amemshukuru pia Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Bernard Membe kwa kufanikisha safari hiyo, na kusema ni ya kihistoria kwani haijawahi kutokea tangu kifo cha Baba wa Taifa.
Kutoka Butiama ujumbe huo wa kimataifa utaelekea Mbuga za Wanyama za Serengeti kwa magari , Olduvai Godge, Lolitoli kuona nyayo za binadamu wa kale na kuishia Ngorongoro. Baadhi ya maeneo mengine watakayotembelea ni Hifadhi ya Manyara kabla ya kuelekea Zanzibar na hatimaye Dar es salaam.    

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...