Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Evans Balama mwenye shati la miraba ya samawati(Katikati) katika picha ya pamoja kabla ya Mheshimiwa Mbunge Joseph Mbilinyi Kuhutubia.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Evans Balama katika jengo la kitega uchumi la OTTU lililopo stendi ya magari madogo ya abiria(daladala), mara baada ya Mbunge Mbilinyi kuhutubia wananchi.
Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi akiwasihi wananchi kuwa watulivu na kwamba mgogoro umekwisha na utatuliwe kisayansi badala ya kisiasa na pia amewapongeza machinga kwa utulivu waliouonesha bila kupora bidhaa madukani.
Wananchi wakirudi makwao kwa furaha baada ya mgogoro uliodumu kwa siku mbili kumalizika, baada ya hotuba ya Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi.
Halaiki ya wananchi waliofika kuusikiliza mustakabali wa wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga kuendelea na biashara zao katika maeneo yao ya awali, wakati utaratibu wa maeneo ya kufanyia biashara ukiandaliwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.Picha zote na: Mbeyayetu Blog.
Malongo anahoji Mbowe anapata wapi nguvu ya kuiamuru serikali. Inashangaza kiongozi wa ngazi ya juu kabisa kimkoa haelewi nguvu ni kitu gani. Hii ndio nguvu mjomba, na imetapakaa nchini kote na hata huko ng'ambo!
ReplyDeleteKazi nzuri wananchi wa Mbeya! Msikubali kuburuzwa kama ng'ombe. Kandoro is out of touch. I hope JK atamuwajbisha.
ReplyDeleteHongera Mheshimiwa Sugu!
washangiliaji tupo tunasubiri tuone mwishowake wa ushabiki tucheke na kuwazomea watakao shindwa maana hatuoni maendeleo zaidi ya uhasama chuki na uroho tu
ReplyDeleteHongera muheshimiwa Mbilinyi kwa busara zako,vurugu zinarudisha nyuma mengi sana.Siku zote ubabe siyo mbinu sahihi ya kutatua matatizo,sijui vyombo vya dora vya nchi yetu vitajifunza lini hili!
ReplyDeleteUMACHINGA: HATA AMSTERDAM -UHOLANZI/ ULAYA UPO::::Hakuna jinsi ndio suluhisho la umaskini kutokana na matatizo ya kiuchumi sio Mbeya au Tanzania bali Dunia nzima...Machinga wawekewe utaratibu ili waendelee na kazi yao, watoe huduma, wachangie kidogo, na wao wajikimu kwa kidogo watakachopata.
ReplyDelete