Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Benki ya NIC Tanzania, James Muchiri (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Mikopo wa benki hiyo Bi Regina Mwengi, Prisalla Karobia na David Muthungu kabla ya kuanza kwa michuano ya gofu iliyoandaliwa na Lions Club na kufanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Benki hiyo ilidhamini kiwanja namba kumi kwa shilingi Milioni 3.5.
Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Benki ya NIC Tanzania, James Muchiri akiangalia mpira baaada ya kuupiga wakati wa Mashindano ya Gofu yaliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana ili kusaidia watu wenye matatizo ya kuona ambapo benki hiyo ilidhamini kiwanja namba kumi kwa shilingi Milioni 3.5.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NIC Tanzania akiwemo Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Benki ya NIC Tanzania, James Muchiri (Katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama Lions Club wakati wa michuano ya Gofu iliyofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ili kusaidia watu wenye matatizo ya macho. Benki hiyo ilidhamini kiwanja namba kumi kwa shilingi Milioni 3.5.

Na Mwandishi Wetu

Benki ya NIC Tanzania kwa kushirikiana na Klabu ya Lions ya Jijini Dar es Salaam wamejitokeza kudhamini mashindano ya mchezo ya Gofu ili kusaidia watu wenye matatizo ya macho.

Katika mashindano hayo benki hiyo imetoa jumla ya Dola za Kimarekani 2000 sawa na Shilingi Milioni 3.5 za Tanzania lengo likiwa ni kuinua afya za wananchi hususani wanaosumbuliwa na matatizo ya macho.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yaliyoshirikisha wachezaji zaidi ya 105, Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa NIC Bank Tanzania James Muchiri amesema ni matarajio yao kwamba udhamini huo utasaidia upatikanaji wa afya bora katika eneo wanalotoa huduma zake.

“Tunatarajia msaada huu ambao ni wa kwanza katika sekta hii ya michezo kupitia Lions Club utasaidia watu wenye matatizo wa macho katika maeneo watakayoenda kutoa huduma hiyo kama ilivyo kawaida ya wana Mzizima,” alisema Muchiri.

Mbali na hayo Mkurugenzi na Mtendaji huyo Mkuu wa NIC Bank Tanzania alisema inakadiwa kuwa zaidi yak watu milioni tatu nchini wanakabiliwa na upofu kutyokana na uwezo mdogo wa kifedha, miongoni mwao wakiwemo wanafunzi.

Kutokana na hilo alisema watahakikisha wanajenga uhusiano mzuri baina yao na Lions Club katika kuunga mkono mchezo wa gofu na kuwahudumia wenye matatizo ya macho.

Nchini Benki hiyo ina matawi Harbour View Tower jijini Dar es Salaam, Mwanza na Arusha huku ikitoa huduma mbalimbali ikiwemo mikopo yenye riba nafuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Idadi kubwa ya mabenki iakisi hali halisi ya mwananchi wa kawaida ,kutoa uwezeshaji kadri iwezekanavyo ili kuvunja kuta zilizopo kati ya matajiri na maskini!

    Huu ndio utakuwa ushindani wa kibiashara wenye tija!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...