Chama cha wamiliki wa vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) kwa kushirikiana na Jukwaa la Wahariri Tanzania leo kimefanya mkutano wa kujadili Amani na mchango wa vyombo vya habari katika kudumisha Amani ambapo mada kadhaa zilijadiliwa katika mkutano huo. Pichani Mwenyekiti wa Taasisi ya Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Reginald Mengi, akifafanua jambo wakati wa mkutano uliofanyika leo katika Hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
Naibu Mhariri Mtendaji wa Free Media, Ansbert Ngurumo akichangia mada katika mkutano wa kujadili Amani na mchango wa vyombo vya habari katika kudumisha Amani ambapo mada kadhaa zilijadiliwa katika mkutano huo,uliofanyika leo jijini Dar.
Mwakilishi wa Africa Media Group Hamza Kasongo akichangia mada katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mhariri wa Gazeti la Uhuru, Jackline Liana nae alichangia mada.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa kujadili Amani na mchango wa vyombo vya habari katika kudumisha Amani ambapo mada kadhaa zilijadiliwa katika mkutano huo..
Baadhi ya Wahariri wakifuatilia kwa makini mkutano huo.


Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jambo Leo, Godfrey Lutego (kushoto), akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, ambaye pia ni Mwenyekiti wa MOAT, Reginald Mengi (kulia) wakati wa mkutano huo wa kukumbushana majukumu ya uandishi wa habari, ikiwemo kufuata maadili ya uandishi, kuwa wazalendo pamoja na kuandika habari za kudumisha amani nchini. Wa pili kushoto ni Jacquline Liana Naibu Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Reginald Mengi (kushoto), akichokoza mada ya umuhimu wa wanahabari kuwa wazalendo wanapoandika habari katika mkutano uliowashirikisha wajumbe wa Jukwaa la Wahariri, Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Absalom Kibanda.
Sehemu ya wahariri watendaji na waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.
ya Katibu Mkuu wa MOAT, Henry Muhanika (kushoto), Mhariri mkuu wa gazeti la Spoti starehe, Masoud Sanani (wa pili kushoto), Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited, Theophil Makunga (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Televisheni ya Mlimani, wakifanya majumuisho mkutano huo.



Katibu Mkuu wa MOAT, Henry Muhanika (kushoto), Mhariri mkuu wa gazeti la Spoti starehe, Masoud Sanani (wa pili kushoto), Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited, Theophil Makunga (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Televisheni ya Mlimani, wakifanya majumuisho mkutano huo.
inabidi muwemakini na kazi yenu kwani kuvunjika kwa amani ya nchi kupo mikononi mwenu
ReplyDelete