Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Salim Ahmed Salim (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Joseph Butiku (wa pili kushoto) wakati akiiwasili kwenye Jumba la Makumbusho ya Taifa leo kwa ajili ya kufungua Mdahalo wa Nafasi ya Umuhimu wa Katiba katika Maisha ya Watanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua Mdahalo wa Nafasi ya Umuhimu wa Katiba katika Maisha ya Watanzania, uliofunguliwa leo katika Jumba la Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa katika mdahalo huo kutoka Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika maonyesho ya Jumba la Makumbusho ya Taifa kuangalia picha za baadhi ya Mashujaa wa Harakati za ukombozi zilizowekwa katika jumba hilo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Salim Ahmed Salim na (kulia) ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Joseph Butiku.
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika jumba hilo na kuangalia baadhi ya picha za matukio zilizowekwa katika jumba hilo kama kumbukumbu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma moja ya kitabu kilochokuwa katika meza ya maonyesho ya vitabu katika Jumba la Makumbusho ya Taifa, baada ya kufungua rasmi Mdahalo wa wa Nafasi ya Umuhimu wa Katiba katika Maisha ya Watanzania, uliofunguliwa leo Novemba 17, katika Jumba la Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi wa Mwalimu Nyerere, Salim Ahmed Salim (kushoto) na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba (katikati) wakiteta jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA) Willbroad Slaa, nje ya ukumbi, wakati Mdahalo wa Nafasi ya Umuhimu wa Katiba katika Maisha ya Watanzania, uliofunguliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katika Jumba la Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. 
Picha zote na mdau Muhidin Sufiani-OMR






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mbona wageni waalikwa wote wamekula chumvi nyingi, au hicho kilikuwa kigezo?

    ReplyDelete
  2. Asante bwana Sufiani.Hiyo picha ya chini kabisa mwisho nimeipenda....inatoa picha fulani kuhusu katiba ya nchi.

    David V

    ReplyDelete
  3. Vichwa vya wazee hao hapo juu in maktaba ya nchi tutwatumie vyema kwenye mchakato huu wa katiba

    ReplyDelete
  4. Hiyo picha ya chini kabisa mimi nimeipenda sana.

    Kama wazee wenye busara na hekima kutoka pande zote za Tanzania wakajumuika na vijana kutoka pande zote na makundi yote ie, walemavu, wafugaji nk. wangekaa bila kujali maslahi maslahi binafsi nadhani mchakato wa katiba ungekuwa na tija zaidi kuliko sasa hivi ambapo limekuwa sualala kisiasa zaidi.

    Inasikitisha sana kuona nchi yangu inakoelekea kwenye siasa na midahalo ya kimakundi, ni hatari sana na wooote tutakuwa wa kulaumiwa sio chama chochote chasiasa wala kundi fulani ni watanzania wooote ndio tutakao ona joto la jiwe lililotokea kwa wenzetu huko.

    Mungu Ibariki Tanzania, mungu ibariki Afrika.

    K.O.R.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...