Marehemu Mzee MSABILA KASSEMBO
Familia ya Marehemu Mzee.MSABILA KASSEMBO wa Tangi bovu,Mbezi Beach Dar es salaam inatoa shukurani za dhati kwa Ndugu,jamaa na marafiki wote ! walioshiriki nao kwenye kipindi kigumu na chenye majonzi makubwa baada ya kupata taarifa za msiba wa Mzazi wao kilichotokea huko Urambo Tabora tarehe 12 October 2011 na kuzikwa huko Itetemia Tabora tarehe 13 October 2011.
Familia inashukuru sana ! Tumepata faraja kubwa sana kwa ushirikiano uliopatikana toka mwanzo wa msiba na mpaka maziko na Tunamuomba Mwenye Enzi wajalie kila la kheri kwa yote Insh Allah !
Familia inawakaribisha kwenye Kisomo cha Arobaini ya Marehemu Mzazi wao kitakachofanyika nyumbani kwa Marehemu Tangi bovu,Mbezi Beach Dar es salaam saa 5 asubuhui siku ya jumapili tarehe 20 November 2011.
Inna Lilahi Waina Ilahi Rajiun !  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...