Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dkt. Hadji Mponda (Mb) akiwa na Maafisa wa Ubalozi Ottawa, Canada. Kutoka kulia ni Bw. Richard Tibandebage, Bibi Nsia Paul, Mhe WaziriDkt. Hadji Mponda, Kaimu Balozi Bw. Joseph Sokoine na Bw. Paul Makelele.

Mheshimiwa Waziri Dkt. Hadji Mponda alikuwa nchini Canada kushiriki mkutano wa ufuatiliaji utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Afya ya Mama na Mtoto (Commission on Information and Accountability on Women's
and Children's Health).

 Mkutano huo ulihudhuriwa na washiriki mbalimbali kutoka kwenye mashirika ya kimataifa, mashirika ya misaada pamoja na Dr. Margaret Chan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mwenyeji wa mkutano huo Mhe. Beverley Oda Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Canada. Kwenye mkutano huo Mhe. 

Waziri Mponda alielezea mafaniko ambayo Tanzania imepata katika sekta ya afya hususan afya Mama na Mtoto, changamoto inazokabiliana nazo na mkakati wa kutekeleza maazimio 11 ya Tume.

Tume hiyo ilikuwa chini ya Uenyekiti wenza wa Mhe. Rais Jakaya M. Kikwete na Waziri Mkuu wa Canada Mhe. Stephen Harper.

Description: https://mail.google.com/mail/images/cleardot.gif

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wewe Sokoine rudi nyumbani ufanye kazi huku, jina na mzimu wa baba yako vitakusukuma kumkomboa mtanzania masikini na anayekandamizwa na ufisadi. Rudi nyumbani! Ingia kwenye sekta ya nishati na madini, afya, elimu, fedha, au wizara ya mambo ya ndani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...